Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Kuna kutoa sare, na kwa mechi kama hizi mara nyingi huishia kwenye sare.
Maneno ya kishabiki haya mzee..
Tuendelee na ushabiki..

Sare inategemea na kipande walichokata, kama wamekata mita 3 hazitoshi kwa sare[emoji1787]
 
Kipindi hiki cha kwanza yanga anastahili/alistahili kufunga
Wamecheza zaidi mpira wa malengo lakini shida ni mtegemewaji wa ufungaji watu walishamlia yamini kuwa hakuna kufunga nayeye kaisha ingia uoga na mguu wake kuwa inaweza mechi ya leo ikamweka nje msimu mzima. Amekuwa muoga wa kujitolea muhanga kwenye matukio ya 50 kwa 50
 
Hii mechi ndio kipimo kwa utopolo kucheza mechi za Caf mwakani. Wanacheza na wa kimataifa.
 
Second half mugalu atupishe
Yani ata ikitokea akaafunga bado kwangu nimesha conclude kua hamna striker humu, Morrison hatakiwi kurudi uwanjani,Sacko kama kawaida yake mbwembwe nyingi bila madhara yoyote.bora hata wacheze akina Mhilu.

Yani huu msimu Simba hatuna watu wakutia mpira kambani kabisa tunapata magoli kwa shida sana.
 
Wamecheza zaidi mpira wa malengo lakini shida ni mtegemewaji wa ufungaji watu walishamlia yamini kuwa hakuna kufunga nayeye kaisha ingia uoga na mguu wake kuwa inaweza mechi ya leo ikamweka nje msimu mzima. Amekuwa muoga wa kujitolea muhanga kwenye matukio ya 50 kwa 50
Sijui anakosa vipi confidence maana anatumia nguvu kubwa kufika na mipkra langoni lakini akifika kwenye 18 ana freeze.

Kuna mpira ambao hata sijaelewa sababu ya ye kushindwa kupiga shuti ilikuwa ni nini matokeo yake mpira unaondolewa na kuwafanya waanze upya

Hapa sasa ndo narudi pale pale kwenye mabishano yetu ya jana, kuwa kama utaendelea kufurahia hizi attempts za bila magoli ambapo zilikuwa na possibility ya kusababisha goli na kuona style hiyo ni bora basi mnasafari ndefu sana
 
Back
Top Bottom