Yanga SC wamefanikiwa 100% kwa hii 'Unbeaten Record' yao na 'Propaganda' madhubuti

Yanga SC wamefanikiwa 100% kwa hii 'Unbeaten Record' yao na 'Propaganda' madhubuti

Akina GENTAMYCINE tukiwa tunasema kuwa kwa sasa Klabu ya Yanga imejipanga vyema hasa kwa upande wa Propaganda muwe mnaelewa/mnatuelewa.

Ukweli ni kwamba Yanga SC siyo wapumbavu kama labda ambavyo tunaweza kudhani kwa wao kuikuza hii 'Unbeaten Record' yao katika Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania.

Yanga SC ambao GENTAMYCINE kama mwamba na mbobezi wa propaganda nawapongeza kwa hili, kwani ili kuonyesha kuwa wamedhamiria lengo lao litimie, hivi karibuni walikuja na kampeni ya kumpongeza Kocha wao Mkuu Nabi dakika ya 43 na kesho wakiwa pale CCM Kirumba Mwanza wakicheza na Geita Gold FC ikifika dakika ya 44 watasimama safari hii kuwapongeza wachezaji wao.

Ukweli ni kwamba kwa Yanga SC kuikuza hii 'Unbeaten Record' yao wameshafanikiwa kwa mafanikio ya kimatokeo ya uwanjani. Kwani tayari hata waamuzi wote watakaowachezesha katika mechi zao za Ligi Kuu wameshaingiwa na uwoga na wao hii 'Unbeaten Record' ipo vichwani mwao.

Hivyo iwe isiwe hawatathubutu kuruhusu Yanga SC ipoteze mechi (ifungwe) mbele yao na watakachokifanya ni kuhakikisha wanaibeba ishinde na kama ikishindikana basi watoke (itoke) sare/suluhu, ila siyo kufungwa ili kujiepusha na lawama ya kuharibu rekodi yao.

Kuna siku hapa hapa GENTAMYCINE nilisema kuwa, Klabu ya Simba imelala na imepwaya mno katika kufanya propaganda na hakina kitengo thabiti cha propaganda (hasa kwa mpira wa Tanzania), lakini kama kawaida sikueleweka. Ila ipo siku tu mtakuwa mnanielewa na kuungana nami kifikra, kimawazo na kimtizamo.

Kwa ambao mnadhani na kujidanganya kuwa ndani ya hii NBC Premier League Klabu ya Yanga itafungwa (itapoteza), mnapoteza muda. Ila kushindwa kwa Yanga SC ni kutoka tu sare/suluhu na kama ni kufungwa basi watafungwa katika Michuano ya CAFCC (ya kimataifa) ambayo huko propaganda yake bado hawajaiwezea/hawajaimudu.

Ila hata huko pia wakipaweza watakuja kuwa imara kuliko hata Simba SC ambao wana uzoefu mkubwa huko (kimataifa).
Mkuu wewe ni msema kweli.
Wapuuzi pekee ndiyo watapingana na hili
 
Linapokuja suala la mashindano ya kimataifa kuna mambo mengi kikosi kizuri tu pekee haitoshi kwa 100%, timu inabidi iwe na DNA ya mashindano husika na iyo kitu uwezi kuinunua inakubidi ushiriki mashindano husika mfululizo ukiwa na focus, unaanguka unainuka unajipukuta vumbi unasubiri msimu unaofata trust me yanga akija kupata DNA ya mashindano ya kimataifa atafanya vzr kuliko simba aliogotea pale pale robo fainali.. uwenda yanga ikawa ndo timu ya kwanza bongo kuingia semi kama sio kuchukua ubingwa kabisa
Acha bange toka 1998 hajapata mbinu
 
Acha bange toka 1998 hajapata mbinu
Nimesema kushiriki ukiwa na focus.. kabla ya uwekezaji wa mo na gsm hizi simba na yanga zilikua zinaenda caf kutimiza wajibu wa kushiriki tu.. mo apewe heshima yake sana ndio wa kwanza kuweka malengo na mikakati ya simba kufanya vizuri mashindano ya kimataifa na wengine wakiwemo yanga, azam na namungo ndo wakaona inawezekana nao wameamka ingawa wameamka tayari simba akiwa ashapiga hatua nyingi mbele yao ila sio mbaya
 
GENTA,

Simba kwenye kitengo cha propaganda wamewapatia njaakalihatari na OKW BOBAN SUNZU sidhani kama upo sahihi kusema kua kwenye kitengo cha propaganda hamna watu.

Ebu pitia nyuzi za hawa watu ndicho utaamini nachokisema.

Anyways!! Mpira wa propaganda haupo siku hizi, Propaganda zimebaki kwenye siasa.
Hawa uliowataja unaona wana Akili?
 
Either ni mjinga au una matatizo ya akili mechi zote za yanga unbeaten zipo na kufungwa Yanga atafungwa tu ni suala la mda, wewe kama mshabiki wa Simba mfano wangekua na unbeaten ya mechi 43 usingeongea tuacheni unafki
Katibiwe Ugonjwa wako wa Akili Oky?
 
Yanga wanaathirika na mentality za wanasiasa. Nguvu kubwa wanayowekeza kwenye 'unbeaten' ndiyo ile ile baadhi ya wanasiasa walikuwa wanawekeza kila aina ya nguvu ili kuhakikisha kila uchaguzi kuanzia urais hadi serikali za mitaa wanashinda 100% maaana wakipoteza mara moja tu wanajua watu watakumbuka udhaifu wao. Ni ushindi ambao hauna uhalisia.
 
Ushindi wa Yanga hauna uhalisia kivip?
 
Yanga wanaathirika na mentality za wanasiasa. Nguvu kubwa wanayowekeza kwenye 'unbeaten' ndiyo ile ile baadhi ya wanasiasa walikuwa wanawekeza kila aina ya nguvu ili kuhakikisha kila uchaguzi kuanzia urais hadi serikali za mitaa wanashinda 100% maaana wakipoteza mara moja tu wanajua watu watakumbuka udhaifu wao. Ni ushindi ambao hauna uhalisia.
Wanaathirika kivipi sasa hapo? Mbona MIKIA ZERO BRAIN.
 
Back
Top Bottom