Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

UPDATES

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo na Yanga inaanza kwa kushambulia lango la Rivers, hata hivyo shuti linapaa juuu.

03' Rivers wanafika lango la Yanga, Adeyum katika jitihada za kuokoa anagongana kichwa na mchezaji wa Rivers

05' Ukwa Nelson anaingia lango la Yanga kwa kuwapunguza msururu wa mabeki, juhudi zake zinaishia hewani.

19' Almanusura Adeyum aweke goli kupitia mpira wa adhabu ndogo kuelekea lango la Rivers

20' Makambo anapiga shuti kali la chini na kutoka nje kidogo ya lango la Rivers

24' Makambo anataka goli kama alilowaweka Zanako lakini inakataa

28' Yakuba anashindwa kuandika bao la kwanza baada ya mpira kuponyoka mlinda mlango kwa kupiga kichwa fyongo

41' Rivers wanaingia kwenye lango la Yanga, shuti linatoka nje ya lango

45+2' Mpira unakwenda mapumziko

51' ⚽Moses anaiwekea Rivers bao la kwanza, Yanga 0-1 Rivers

64' Feisal Salum anapata nafasi ya kusawazisha baada ya Makambo kuuruka mpira lakini anapaisha juuu

=========

View attachment 1934361



Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) leo watashuka kwenye dimba la uwanja wa Benjamin Mkapa kupambana na timu ya Rivers United katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya mashindano hayo

Baada ya mechi hii, timu hizo zitarudiana tarehe 19/09/2021 ili kuweza kupata mshindi atakayefuzu kwenye hatua inayofuata

Ungana nami nikikuletea kinachojiri katika mpambano huo

#RetunsOfChampions

Kikosi Cha Yanga

1. Diarra
2. Kibwana
3. Adeyum
4. Job
5. Mwamnyeto
6. Mukoko
7. Jesus
8. Mauya
9. Makambo
10. Feisal
11. Yacouba
Manara afukuzwe
 
Back
Top Bottom