Yanga yagomea mechi kupigwa saa 1, mechi yaahirishwa

View attachment 1777519
View attachment 1777520
My Take
Kama TFF haikushirikisha timu zote ni wapumbavu wa kudumu. Kwa nini walipanga mechi saa 11 wakijua kuna changamoto
Hii si amri ya TFF ni wizara ya habari na michezo. Kuna siasa zinapenya hapa na hazikutumika busara. Kama kuna mtu inabidi awepo kwa maamuzi ya ghafla si wangeongea na timu zote tu. TFF wametii mamlaka kwa mujibu wa barua yao kujivua lawama.
 
Tff wanawahujumu yanga,


Kwanini wawapangie mechi za usiku ili hali wanajua fika yanga hawachezi mechi za kimataifa muda mrefu hivyo hawana uzoefu na mipira ya usiku......! Hata uwanja tu wa Ben Mkapa ni shida nadhani wangepanga mechi za yanga zichezwe uwanja wa mabatini kule kwa Masau Bwire.


Ila jamani, masaa matatu hata kwa mashabiki tu ni tafrani, sijui aliyefanywa haya maamzi Kama Yuko timamu au labda alikuwa gerezani ameachiwa Leo ndo anashituka kuona ratiba inasema 11.. !
 
Mimi mnyama lakini nawapendaga sana wananchi hawapepesi macho. Well done Dar young Africans. Wekeni historia vizuri itawakumbuka daima.
Wanyama tuko vizuri uwanjani ili kwenye kugongana na serikali hapana asee. Mwambieni jk amueleze vizuri mama kuhusu utaratibu ulivyo.
 
Ushabiki maandazi sisi tunaita usela mavi. Sijui umeandika kitu gani
 
Hii si amri ya TFF ni wizara ya habari na michezo. Kuna siasa zinapenya hapa na hazikutumika busara. Kama kuna mtu inabidi awepo kwa maamuzi ya ghafla si wangeongea na timu zote tu. TFF wametii mamlaka kwa mujibu wa barua yao kujivua lawama.
Hapo ndipo TFF walipoonyesha udhaifu kwa hiyo wanyewe walishindwa kuchakata taarifa na kutoa sababu konki zilizofanya mechi ipangwe saa 11 awali? Kwa hiyo wanatawaliwa na wana siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…