Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Kwa hiyo klabu nyingine zitabaki kutoa macho zikiona yanga na simba wanavyopepea kwa nn azam media assiinue klabu yake ambayo kila mwaka ni wasindikizaji tu tutabaki kuwa na klabu 2 tu simba na yanga ndio maana soka la bongo haliendelei vipi kuhusu mtibwa mbeya city kagera sugar na klabu nyingine kwani wao hawapendi kuonekana.
Ni biashara. Lengo ni faida.
Wakuze timu zao kwanza. Mbaya walikuwa wanawacheka Yanga akipitisha bakuli Sokoine. Micha go na kubwa kuliko ilizalisha 1.6bn.
Leo Gor Mahia wameanza bakuli.
Sasa timu watu hawainvest, haikui halafu unataka Azam awake mzigo apate hasara?
 
Swali gani?
Social media na traditional media zina conflict, labda zote ziwe kampuni Moja. Kunakuwaga na give and take not give and give
Kama hujawlewa tambaa tu Hamna haha ya kukubaliana.
Asante kwa jazba. Sitoendelea kujadili lolote nawewe.
 
Kwani MO ana TV?
Hapo Simba inaingia Mkataba na Azam TV na sio METL na SSB
Watu wanachanganya sana mambo, yaani wanadhani kama Mo na Bakhressa ni washindani kwenye kuuza juisi na unga wa ngano, basi wanashindana kwenye kila kitu ikiwemo Media.
 
Hakika Yanga mmewapiga Bao Simba kwa huo mkataba mnono wa zaidi ya Billioni 34.
Hongera nyingi kwenu.

Nina uhakika kuanzia sasa mtakuwa na timu Bora kabisa katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Tunasubiri matunda ya haya mafanikio mliofikia.

Ile lialia ya Bakuli natumai hatutaisikia tena.
Una uhakika kuwa Simba hawatapewa?
 
Wewe fuatilia mgogoro wa Simba na AZAM kuhusu Simba Day Youtube clip.

Usipende ubishi usio na manufaa.
Na Simba hawataki achia Youtube Channel yao ndo maana hadi sasa hakijaeleweka, ukiona wameelewana jua hela imeongezwa
 
Unabisha ili ubishe tu
Wewe ndio unabisha kumtetea mo tu,mkataba huu si mara ya kwanza kuiingia sema umeongezeka thamani ya pesa na baadhi ya vitu,kikubwa hapo mo anataka kununua hilo timu kwa b 20 na kagoma kutoa,hii ya azam kwa miaka 10 bln 34 anaona aibu maana itazua hisia za watu kutaka apande dau kwenye uwekezaji pia ambapo b 20 alisema ni pesa nyingi sana huku thamani ya mikia b 3 na nyie mkakubali timu lenu lina thamani ya b 3!

Screenshot_20210709-085350_Instagram.jpg
 
Kampuni Moja.
We vipi? Hivi mbona mnalazimisha vitu vipo wazi?
Kulikuwa na mgogoro wa Simba Tv(Azam) na Simba YouTube.
Wewe unafikiri kwa nini? ... Same content different media house . Tofauti na same media house
Dah!

Naomba nikukumbushe,ulisema hapa Azam hawako kwa Social Media kabisa wanatumia Traditional way,ndiyo tukakuuliza kama Azam hawapo kwa Social Media platforms, hizo Account zao huko IG,Twitter na FB ni za nini? Sasa hivi unatwist tena jibu kuwa hao ni Kampuni moja.Kwa hiyo tunakubaliana ulitaka kupotosha kuwa Azam hawatumii Social Media Platforms?
 
Nani kakuambia ushabikie Simbilisi? Ona Sasa, bingwa lakini una hasira .
Mwishowe kaniki na usembe usoni, unafanya kupaa na fagio Dar-Kisiju- Kivinje.

Nilidhani unachangia hapa kwa kutumia nguvu ya hoja,kumbe umetanguliza Unazi wako wa ki Utopolo[emoji3]
 
Sasa kama ya yanga hayanihusu wewe ya simba yanakuhusu vipi hadi unauliza simba ina uwanja?
Nakuuliza baada ya wewe kuuliza kwanini mimi na wewe nani aliyeanza kuuliza ya mwenzie??
 
Kwa mkataba wa 34 B wa TV right wa Yanga naweza kuinunua Simba ( 49% shares). Mfano Naenda Bank nakopa mkopo wa 21 Billion for 15 years repayment ambapo dhamana ni Contract ya Azam tv na hizo shares pia malipo ya mwezi ambayo azam tv atatakiww kulipa ndio rejesho la huwo mkopo. Ndio maana nasema Mo amewaibia sana Simba haiwezekani ukapata umiliki kwenye Club kubwa kama Simba kwa 20 Billion tena ya mkopo…. Mpaka leo Mo ametengeneza pesa nyingi sana kupitia Mo energy product for free sana
 
Hawa watu hawajui kuwa hela aliyotumia Abro kuinunua Chelsea ni ndogo kuliko Mkataba wa Chelsea na NIKE au Hyundai
Mtu mwenye akili timamu na aneelewa maana ya biashara hawezi kubisha juu ya hilo,maana kiuhalisia biashara inatakiwa iwe hivyo.

Hivi ununue club kwa hela kubwa kuliko,mapato ya club alafu faida itapatikana wapi? Ni sawa na mtu anunue kitu 600M Ili aingize faida ya sh 50 kwa siku.
 
Back
Top Bottom