Kwanin unaamin kitu unachoamini ndo sahihi, wenzako wanasema ni kinyume na katiba na tamaduni zao we unabisha nin mke,
Mi siwezi kuamini alichosema Mwakalebela kwa sababu Kwenye press conference hiyo hiyo amedanganya kua TFF waliwahujumu Kwenye siku ya mwananchi wakaweka Mechi ya marudiano na Kenya siku ya jmosi ambayo ni siku moja kabla ya siku ya mwananchi.
Tujuulize hivi mechi ya Chan qualification wanapanga TFF au CAFU.
Pili, Kwenye hiyo mechi Kenya ndo alikua mwenyeji, Je, TFF walihusikaje kusema mechi hiyo iwe jmosi kwa ajili ya kuwarubuni Yanga.
Hili la kusema katiba yao hairuhusu, Je, hii sheria ya kua kama timu itagomea nembo ya mdhamini imetungwa baada ya Vodacom kuingia au ilikuwepo muda?
Kama ilikuwepo kwa nini Yanga wasubiri saizi mdhamini amepatikana ndo wasema hawatavaa?
Kwa nini wasingeipinga mapema kabla ya kutokea?
Kwenye hili nataka nione ka sheria zinatungwa kwa ajili ya kuendesha mpira wa Tanzania au kwa ajili ya timu ndogo tofauti na Simba na Yanga.
Chama cha soka Italy hakikuangalia ukubwa wa Juvetus, ila walishushwa kwa sheria.