Yanga yamshitaki Feisali Salum kwenye kamati ya nidhamu

Yanga yamshitaki Feisali Salum kwenye kamati ya nidhamu

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Kamati ya Sheria na Nidhamu ya Young Africans imemuelekeza Feisal kuwasilisha utetezi wake juu ya tuhuma zinazomkabili ndani ya siku 7.

Pia Kamati imemuelekeza kuhudhuria Kikao cha Kamati ya Sheria na Nidhamu kitakachosikiliza mashtaka dhidi yake jana tar 24 Mei 2023 pamoja na muwakilishi wake (endapo angependa kufanya hivyo) ili kusikiliza yeye pamoja na mlalamikaji na kufanya maamuzi juu ya tuhuma zinazomkabili

Endapo atashindwa kuwasilisha utetezi wa maandishi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndani ya muda au kutofika kwenye kikao, basi kikao kitaendelea bila uwepo wake.

Screenshot_20230525-113105.png
Screenshot_20230525-113120.png
 
Naskia kuna tetesi dogo kapeleka kesi CAS
Lab
Hanyanyasiki anajua anachofanya. Wanyonge ndo wananyanyasika huyu haonekani kama ni mnyonge ana nguvu inayompa ujasiri wa kuwavimbia Yanga.
Mtu mkubwa sana huyo, hawezi kunyanyasika. Wanamsingizia tu.
Kwa style aliyoitumia huyu hata waliomdanganya hawatamtaka tena, sanasana watamuunganishia akachezee Mlandege au Small Simba
 
Ameshamaliza zake za sakafuni, ngoja sasa waanze naye.
Ni mchezaji wao aliyamua kujinyanyasa, itabidi anyanyasike tu, hakuna namna.
Ingekuwa Yanga inamfukuza bila maslahi tungesema ananyanyasika. Huyu hataki kukaa na Yanga, Hataki mshahara wa Yanga, Hataki hata kusikilizana nao. Sioni manyanyaso hapo zaidi ya jeuri. Na hakuna mtu ataleta jeuri bila maslahi.
 
Ameshamaliza zake za sakafuni, ngoja sasa waanze naye.
Ni mchezaji wao aliyamua kujinyanyasa, itabidi anyanyasike tu, hakuna namna.
Kipindi kile ilikuwa kila Yanga anapokaribia kwenye mechi kubwa halafu ikaonekana Feisali ameenda TFF kuhusu swala lake na Yanga, ikitafsiriwa kama njia ya kuwatoa Yanga mchezoni

Leo Yanga wenyewe ndio wameanza uchokonozi bila kujali kama wapo kwenye wiki ya kujiandaa na mechi kubwa.
 
Hanyanyasiki anajua anachofanya. Wanyonge ndo wananyanyasika huyu haonekani kama ni mnyonge ana nguvu inayompa ujasiri wa kuwavimbia Yanga.
Masponsor wanampa kiburi,ila kuondoka kwake hakujaweza kuharibu move ya Yanga kuelekea kuchukua Vikombe,so wampe soft exit akapambanie maisha mbele.
 
Hanyanyasiki anajua anachofanya. Wanyonge ndo wananyanyasika huyu haonekani kama ni mnyonge ana nguvu inayompa ujasiri wa kuwavimbia Yanga.
Hersi alisema Yanga ilimboreshea maslahi yake kutoka 1.5M hadi 4M.

Na anakiri kuwa Feisali ni mchezaji ambaye hajawahi kuwa na nidhamu mbovu au jambo lolote la kutilia shaka kwenye taaluma yake

The question is, what changed him?
 
Lab

Mtu mkubwa sana huyo, hawezi kunyanyasika. Wanamsingizia tu.
Kwa style aliyoitumia huyu hata waliomdanganya hawatamtaka tena, sanasana watamuunganishia akachezee Mlandege au Small Simba
CAS wakitoa majibu kuwa maamuzi yaliyotolewa na TFF hayakuzingatia kanuni za FIFA mtasemaje?
 
Mjini kuna mambo mengi sana huwezi kuamini kwamba mtu anayejiita tajir namna moja anahisika na huu upuuzi wa huyu kijana
 
Lab

Mtu mkubwa sana huyo, hawezi kunyanyasika. Wanamsingizia tu.
Kwa style aliyoitumia huyu hata waliomdanganya hawatamtaka tena, sanasana watamuunganishia akachezee Mlandege au Small Simba
Mtu mzima huyo. Anajua anataka nini. Kwani Yanga club ndogo? Inakubembeleza njoo tuongee hutaki? Mwajiriwa gani hataki mshahara? Ukiona mwajiriwa anakataa mshahara basi anauhakika kuna sehemu nyingine amepata kikubwa zaidi.
 
CAS wakitoa majibu kuwa maamuzi yaliyotolewa na TFF hayakuzingatia kanuni za FIFA mtasemaje?
Maadam mkondo wa sheria na utaratibu utafuatwa na bila shaka wakiainisha hayo mapungufu kutakuwa hakuna namna. Itabidi Yanga kujifunza, si kila wakati au kila hatua utakuwa mshindi. Kuna kipindi unaondolewa kabisa kwenye game, iwe kihalali au kidhuruma, halafu njia ileile uliyodondoshewa ikakupeleka kwenye ushindi.

So, itabidi Yanga ikubali matokeo, maana nguvu watakayozidi kuitumia kupambana na huyu itawatisha wachezaji wenzake kule alipowaacha kiasi cha kuanza kujihisi na wao hawapo salama.
 
Back
Top Bottom