Yanga yamshitaki Feisali Salum kwenye kamati ya nidhamu

Hersi alisema Yanga ilimboreshea maslahi yake kutoka 1.5M hadi 4M.

Na anakiri kuwa Feisali ni mchezaji ambaye hajawahi kuwa na nidhamu mbovu au jambo lolote la kutilia shaka kwenye taaluma yake

The question is, what changed him?
Mara nyingi sana maslahi ndo humbadili mtu. Huenda hiyo 4m aliridhika nayo kabisa mpaka alipotokea mtu na m500 akamkabidhi na kumwambia ukifanikiwa kuvunja mkataba na Yanga ntakulipa mshahara wa m20 kwa mwezi. Huenda lakini.
 
Mara nyingi sana maslahi ndo humbadili mtu. Huenda hiyo 4m aliridhika nayo kabisa mpaka alipotokea mtu na m500 akamkabidhi na kumwambia ukifanikiwa kuvunja mkataba na Yanga ntakulipa mshahara wa m20 kwa mwezi. Huenda lakini.
Jambo ambalo ni kawaida kwenye mpira wala halikupaswa kuchukuliwa kama uadui kama ambavyo lilipofikia.

Ila bado kuna mambo mengi yanasemwa ambayo bado hayajathibitishwa kuhusu tuhuma za mchezaji kunyanyaswa

Na ndio maana kwa madai yake kupitia mawakili wake anasema hata Yanga wakisema wanamlipa pesa kama hiyo bado hawezi kukubali kurudi
 
Nyuma ya huu upuuzi wote yupo Yusufu Bakresa. Kiburi na Jeuri ya fedha ndizo zilizopelekea Feisal na wazazi wake kuchanganyikiwa.
Sasa anajifunza kua sio marazote fedha ikaweza kununua Kila kitu.
Yanga wameamua kumshikisha Adabu Yusufu ila bahati Mbaya Feisal ndio atakua mwenye maumivu juu ya ubabe unao endelea.
 
Kweli.

Sasa ni fimbo ipi kamati ya Yanga wataitumia kumchapa nayo iwapo fedha zao hazitaki?

Labda wakaishawishi TFF imfungie kucheza mpira kipindi kirefu otherwise hakuna watakalofanya lenye madhara zaidi ya hili la kumbainia kuondoka mpaka mkataba uishe.
 
Sasa kama Fei amewezeshwa kwa fedha ya maana maumivu atayatoa wapi? Kwani mpira watu si wanacheza ili wapate fedha?

Labda afungiwe kucheza mpira kwa kipindi kirefu tutasema amewezwa sababu hata kama kapewa pesa nyingi haziwezi lingana na future ambayo alikuwa ameshaitengeneza.
 
TFF nayo sio ya kuiamini sana kwenye kufuata sheria
 
Reactions: Tsh
TFF nayo sio ya kuiamini sana kwenye kufuata sheria
Wakisema afungiwe miaka 2 kwenda mbele kujihususha na michezo hapo atakuwa kakomolewa maana 2 years bila kucheza obvious possibility ya kupotea moja kwa moja ni kubwa.
 
Pesa siyo kila kitu!
Fei anayelipwa ml 4 kwa mwezi kapata wapi ml 100 za kuwalipa yanga?
Anapata wapi kiburi cha kublock account yake ili mshahara wa yanga usiingie kwake?
Asichokijua ni kwamba hata pesa ikiwa rejected kumbukumbu zinabaki kuwa ulilipwa ila account ili reject
Hapa ndipo shule inapoingia sasa!
Hakuna sehemu azam walishawahi kuja mbele na kusema wanamtaka fey lazima kuna wahuni wa hapo kariakoo wapo nyuma yake huyu dogo
Walipofanikiwa kwa morison wakaona yanga ni timu local ya kuchezea
Sasa pale hakuna mwakalebela wala mshindo msola .twende kazi
 
Haya uliyoongea yote yanaonyesha Fei hana shida na fedha. Ameshawezeshwa kifedha.

Kama upo sahihi basi Furaha yako itakuwa halisi iwapo tu Fei atafungiwa kucheza soka otherwise hakuna adhabu itakayomkomoa ili ufurahi.
 
Haya uliyoongea yote yanaonyesha Fei hana shida na fedha. Ameshawezeshwa kifedha.

Kama upo sahihi basi Furaha yako itakuwa halisi iwapo tu Fei atafungiwa kucheza soka otherwise hakuna adhabu itakayomkomoa ili ufurahi.
Hata hakimu anapohukumu case anasema. " unakwenda jela miaka 60 ili iwe fundisho kwa wengine" so mm furaha yangu afungiwe ili wengine wajifunze kuheshimu mikataba yao.
Mane alifanya kazi kubwa sana Liverpool lakini alikuwa analipwa mshahara kiduchu kuliko hala chamberlain ulishasikia Mane amegoma pale Liverpool? Aliheshimu mkataba hadi mwisho ulivyoisha akahamia bayern Munich huo ndiyo weledi siyo mtu alete uhuni uhuni tu
 
Tukishachukua kombe la CAFCC ndio tutamuacha huyo mjinga aende anakotaka saa hizi tuko bize ati.
 
Sijajua uelewa wako ukoje katika uendeshaji wa taasisi, ila nikusaidie tu kuwa taasisi inakuwa na watu/ vitengo vingi
 
Sidhani, wakati mwingine ushabiki unaletaga upofu tu. Akirudi Yanga akapokelewa na zawadi ya mshahara mnono concept yako ya iwe fundisho kwa wengine pengine ukaipuuza na kumshangilia kama kina Morison.
 
Sidhani, wakati mwingine ushabiki unaletaga upofu tu. Akirudi Yanga akapokelewa na zawadi ya mshahara mnono concept yako ya iwe fundisho kwa wengine pengine ukaipuuza na kumshangilia kama kina Morison.
Sitashangazwa hata kidogo. Hata Morriston haikunishangaza. Wala sijawahi mshangilia Morriston. Mm nazungumzia mantiki ya mkataba na uvunjaji wake. Ni sawa na wewe uache kwenda kazini kisa unalipwa mshahara mdogo???
Ulipokuwa shule ulifundishwa kwamba ili kuvunja mkataba/kuboresha unatakiwa kutoroka kazini???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…