Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Jize one

Member
Joined
Jul 8, 2025
Posts
25
Reaction score
29
Akizungumza na jembe FM Bi jasmine Razack ambaye ni msimamizi wa mshambuliaji wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania Clement Mzize amesema klabu ya yanga imegoma kumwachia Mzize kujiunga na klabu ya Al Masry kwa ofa waliyokuja nayo huku Yanga wao wakitaka kiasi Cha dola million moja ili waweze kumuachia mshambuliaji wao huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri uliomalizika.
Bi jasmine Razack ameongeza kusema kuwa klabu ya yanga ni kama imeamua kufanya kwa makusudi kumzibia milango Mzize ya kwenda nje ya mipaka ya Tanzania akitolea mfano kusema kuwa mbona hapo nyuma walikubali kumuachia mshambuliaji wao hatari Fiston kalala Mayele kwa dau la dola laki Tano (500,000) aweze kujiunga na Pyramids Fc kwanini isiwe kwa Mzize
Ikumbukwe kuwa Jasmine Razack alihusika katika sakata la mgogoro kati ya yanga na Feisal salum kabla ya kujiunga na azam fc.
Je unadhani klabu ya yanga Ina shida kwenye kuachia wachezaji wake kwenda kutafuta changamoto nyingine hasa nje ya nchi? au Wasimamizi wa wachezaji hao ndo watangeza migogoro na klabu ya yanga kwa manufaa yao binafsi?
Screenshot_20250809-141751.png
 
Acheni mihemko. Yanga ndiyo iliyo muajiri Clement Mzize, na ndiyo yenye haki ya kumuuza kwa bei ambayo wanaona inafaa.

Vipi ikitokea timu ina dau ambalo Yanga wataliridhia? Ni lazima auzwe huko Al Masry? Ni lazima Mzize auzwe kwa dola laki 5, kwa sababu Mayele aliuzwa Pyramid kwa dau hilo?

Siyo kwamba huyo Jasmine ana nongwa? Kwani ni lazima mchezaji mwenye mkataba kuuzwa kwenye timu nyingine inayomhitaji? Alisajiliwa Yanga ili auzwe, au lengo la kwanza ni kucheza mpira na kuiletea timu makombe? Ni kwa nini Yanga isiwe na haki ya kuamua kumuuza mchezaji kwa pesa wanayo ona inafaa, badala ya wakala kuleta mashinikizo yasiyo na tija kwa sababu tu ya 10%?
 
Kwanza wanafananishaje dau la wachezaji wawili wenye umri tofauti kabisa?
 
Huyo Jasmine, mwambie kama ni rahisi aanzishe timu yake awe anauza wachezaji kwa bei anayoitaka. Yeye kama meneja kweli akatafute timu huko zenye kummudu.
 
Jasmine ndiye bure kabisa; hajui kumwakilisha mteja wake, anachojua sana ni kupambana na vilabu badala ya kukaa ana kuongea nao. Kwa hili alitakiwa aongeee na yanga kwa vile ndio wanaommiliki Mzize, lakini yeye anataka kulazimisha Yanga imuachie Mzize kulingana na matakwa yake mwenyewe Jasmine ili apokee kamisheni yake. Huyu mama hawasidii vijana wetu, ila anajisaidia mwenyewe. Kwenye busara tulifundishwa kuwa unapopanda mlimani, wasalimie vizurim unaokutana nao njiani kwani utaweza kukutana nao tena wakati unatelemka. Yeye anatukana anaokutana nao wakati anapanda mlimani!
 
Back
Top Bottom