Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Akizungumza na jembe FM Bi jasmine Razack ambaye ni msimamizi wa mshambuliaji wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania Clement Mzize amesema klabu ya yanga imegoma kumwachia Mzize kujiunga na klabu ya Al Masry kwa ofa waliyokuja nayo huku Yanga wao wakitaka kiasi Cha dola million moja ili waweze kumuachia mshambuliaji wao huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri uliomalizika.
Bi jasmine Razack ameongeza kusema kuwa klabu ya yanga ni kama imeamua kufanya kwa makusudi kumzibia milango Mzize ya kwenda nje ya mipaka ya Tanzania akitolea mfano kusema kuwa mbona hapo nyuma walikubali kumuachia mshambuliaji wao hatari Fiston kalala Mayele kwa dau la dola laki Tano (500,000) aweze kujiunga na Pyramids Fc kwanini isiwe kwa Mzize
Ikumbukwe kuwa Jasmine Razack alihusika katika sakata la mgogoro kati ya yanga na Feisal salum kabla ya kujiunga na azam fc.
Je unadhani klabu ya yanga Ina shida kwenye kuachia wachezaji wake kwenda kutafuta changamoto nyingine hasa nje ya nchi? au Wasimamizi wa wachezaji hao ndo watangeza migogoro na klabu ya yanga kwa manufaa yao binafsi?View attachment 3436663
Masaa 72 tu yakiisha story za Yanga kuichangia CCM zitaisha na wananchi wataanza jadili kuhusu Mzize. Naipenda nchi yangu
 
Back
Top Bottom