Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Yanga yamuwekea ngumu Mzize kwenda Al-Masry

Eng kwa hili anaferi sana hataki kuwapa fursa vijana huko nje huyo Mzize angemuuza kitambo huko Wydad anataja dau kubwa kama anamuuza Messi..
Al Masr dirisha limeshafungwa, ofa yao ndogo na ni timu ya kawaida, ipo ofa ya Qatar Yanga wameikubali ila Jasmine hataki anamwambia Mzize asubiri hadi afike miaka 32, na pia kama Yanga wanapata 900k dola basi mzize apple dola laki3, sasa mwana Yanga mwenzangu Qatar na Misri we unaona bora wapi?

Mshahara mzize Qatar ni dola elf 20 kwa mwezi
 
Huyo mama ndio tatizo kubwa. Ametumwa na hiyo timu ili apeleke presha Yanga ikubali ofa mchele. Yanga inataka kumuuza mchezaji kwenye timu itakayoleta ofa kubwa zaidi. Jasmine anataka Mzize auzwe kwa bei kama ya Mayele. Shenzi kabisa

Nyie makolo mnaosema Yanga anabania wachezaji hili ni fundisho kwenu nyote namna biashara zinafanyika, sio unaachia achia tu wachezaji kizembe kwa bei chee. Huyu Mzize anayeliliwa hivi bila Yanga hii angekua wapi? Hapa hata viongozi wenu wanajifunza namna ya kuwa na msimamo kwenye biashara
 
Al Masr dirisha limeshafungwa, ofa yao ndogo na ni timu ya kawaida, ipo ofa ya Qatar Yanga wameikubali ila Jasmine hataki anamwambia Mzize asubiri hadi afike miaka 32, na pia kama Yanga wanapata 900k dola basi mzize apple dola laki3, sasa mwana Yanga mwenzangu Qatar na Misri we unaona bora wapi?

Mshahara mzize Qatar ni dola elf 20 kwa mwezi
Ndugu hizi habari unatoa wapi? Kwa huo mshahara si bora atafute timu hapahapa Africa imlipe mshahara kama huo.
 
Acheni mihemko. Yanga ndiyo iliyo muajiri Clement Mzize, na ndiyo yenye haki ya kumuuza kwa bei ambayo wanaona inafaa.

Vipi ikitokea timu ina dau ambalo Yanga wataliridhia? Ni lazima auzwe huko Al Masry? Ni lazima Mzize auzwe kwa dola laki 5, kwa sababu Mayele aliuzwa Pyramid kwa dau hilo?

Siyo kwamba huyo Jasmine ana nongwa? Kwani ni lazima mchezaji mwenye mkataba kuuzwa kwenye timu nyingine inayomhitaji? Alisajiliwa Yanga ili auzwe, au lengo la kwanza ni kucheza mpira na kuiletea timu makombe? Ni kwa nini Yanga isiwe na haki ya kuamua kumuuza mchezaji kwa pesa wanayo ona inafaa, badala ya wakala kuleta mashinikizo yasiyo na tija kwa sababu tu ya 10%?

Akianza kucheza ovyo msilalamike, mkasema emehongwa, mchezaji Huwa alazimishwi anashawishiwa. Kama mwenyewe anataka kuondoka ya nini kumzuia. Huo ndo mpira. Hakuzaliwa yanga mwcheni aende anakotaka.
 
Huyo maza ni kichomi...

Kila dili analokuwepo lazima liwe na mauzauza...
 
Akianza kucheza ovyo msilalamike, mkasema emehongwa, mchezaji Huwa alazimishwi anashawishiwa. Kama mwenyewe anataka kuondoka ya nini kumzuia. Huo ndo mpira. Hakuzaliwa yanga mwcheni aende anakotaka.

Mchezaji hawezi shindana na timu, ukicheza hovyo unakula benchi kiwango kinashuka...
 
Al Masr dirisha limeshafungwa, ofa yao ndogo na ni timu ya kawaida, ipo ofa ya Qatar Yanga wameikubali ila Jasmine hataki anamwambia Mzize asubiri hadi afike miaka 32, na pia kama Yanga wanapata 900k dola basi mzize apple dola laki3, sasa mwana Yanga mwenzangu Qatar na Misri we unaona bora wapi?

Mshahara mzize Qatar ni dola elf 20 kwa mwezi
Maisha ni pesa mkuu kama hiyo dola analipwa hapo Chunya aende huko Qatar ni mbali unawezaje kukataa hela nyingi kwa kutaka kutengeneza sifa tu..
 
Akianza kucheza ovyo msilalamike, mkasema emehongwa, mchezaji Huwa alazimishwi anashawishiwa. Kama mwenyewe anataka kuondoka ya nini kumzuia. Huo ndo mpira. Hakuzaliwa yanga mwcheni aende anakotaka.
Mchezaji professional ukifanya hivyo kwenye timu ambayo inakulipa mshahara kila mwezi, na una mkataba nayo! unaonekana huna akili timamu.
 
Jasmine ndiye bure kabisa; hajui kumwakilisha mteja wake, anachojua sana na kupambana na vilabu badala ya kukaa ana kuonea nao. Kwa hili alitakiwa anaongeee na yanga kwa vile ndio wanaommiliki Mzize, lakini yeye anataka kulazimisha Yanga imuachie Mzize kulingana na matakwa yake mwenyee Jasmine ilia apokee kamisheni yake.
Kuna mawakala wanamiliki Wachezaji yeye anashindwa nini,?
 
Akianza kucheza ovyo msilalamike, mkasema emehongwa, mchezaji Huwa alazimishwi anashawishiwa. Kama mwenyewe anataka kuondoka ya nini kumzuia. Huo ndo mpira. Hakuzaliwa yanga mwcheni aende anakotaka.
Haya ni maoni ya asiyejua chochote kuhusu biashara ya Wachezaji. Brentford juzi tu wametuonyesha nguvu ya umiliki Kwa Mbeumo wakati mchezaji alishakubaliana Kila kitu na Man U. Wamebargain mpaka kiwango chao walichotaka kilipotimia. Kusema mchezaji akitaka anaondoka umetumia Kanuni ipi au ushabiki?
 
Akizungumza na jembe FM Bi jasmine Razack ambaye ni msimamizi wa mshambuliaji wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania Clement Mzize amesema klabu ya yanga imegoma kumwachia Mzize kujiunga na klabu ya Al Masry kwa ofa waliyokuja nayo huku Yanga wao wakitaka kiasi Cha dola million moja ili waweze kumuachia mshambuliaji wao huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri uliomalizika.
Bi jasmine Razack ameongeza kusema kuwa klabu ya yanga ni kama imeamua kufanya kwa makusudi kumzibia milango Mzize ya kwenda nje ya mipaka ya Tanzania akitolea mfano kusema kuwa mbona hapo nyuma walikubali kumuachia mshambuliaji wao hatari Fiston kalala Mayele kwa dau la dola laki Tano (500,000) aweze kujiunga na Pyramids Fc kwanini isiwe kwa Mzize
Ikumbukwe kuwa Jasmine Razack alihusika katika sakata la mgogoro kati ya yanga na Feisal salum kabla ya kujiunga na azam fc.
Je unadhani klabu ya yanga Ina shida kwenye kuachia wachezaji wake kwenda kutafuta changamoto nyingine hasa nje ya nchi? au Wasimamizi wa wachezaji hao ndo watangeza migogoro na klabu ya yanga kwa manufaa yao binafsi?View attachment 3436663
Hapa Bongo na wivu unahusika.

Huyu msomali wenu ni roho mbaya nadhani mnakumbuka Ile ya Feitoto.

Kama Nzinze/Wakala wake wanataka kutoka wajatoboe wamuombe Rais SSH aingilie kati vinginevyo ndio hivyo.
 
Nimefuatilia hili swala nimegundua kwamba watanzania tulio wengi tuna shida katika fikra zetu... Inakuaje mtu unasikiliza maelezo ya upande mmoja na kutoa hukumu?

Ukiwasikiliza yanga pia wanadai walipata offer nzuri na wakawa tayari kumuachia mzize lakini management ya mchazaji wakagoma wakisema mshahara wa mchezaji ni mdogo.. kuna story ndefu kidogo hapo ila point yangu tuwe tunajifunza kuskiliza pande zote kabla ya kutoa hukumu.
 
Hersi Said.

Nzinze kama ana akili aombe Msaada wa Rais hata Kwa njia ya media.Hapo Kuna wivu wa maslahi nothing else
Ungebaki tu kwenye siasa,Mpira sio mambo yako,..Jana tu Newcastle wamemwambia isak kua HAUZWI Liverpool hata waje na dollar billion, point hapo ni kwamba mchezaji akiwa na mkataba ni Mali ya club,club ndio itaamua auzwe au abaki,na Kwa kiasi gani,.kwanini suala hili gumu sana kwenu kuelewa??
 
Wachezaji wetu wanaotafuta maisha Mazuri zaidi ambayo Yanga na Simba hawawezi kuwapa.

Pia kama Nchi tunataka wachezaji wakapate exposure Nje Ili tuwe na Timu nzuri ya Taifa ,ligi ya ndani dhaifu haitupi wachezaji classic.

Nasisitiza Nzinze amtafute Rais Ili aingilie kati huu wivu,huyo Hersi hata salary mil.75 hapo Kwa GSM so anaweka ngumu kisa wivu.

Thlikes of Feitoto
 
Wewe ni mpumbavu kabisa... Yaani unataka timu ziwe daraja tu la kutengeneza wachezaji wanufaike wako kuliko timu?, wakala hana mamlaka ya kumlazimisha mchezaji auzwe mahali fulani?, hana umiliki wowote kwa mzinze zaidi ya kumwakilisha kimkataba tu. Acheni mihemko ya kisengelema.
 
Mpumbavu ni wewe ,Tanzania hakuna Timu za maana za kuwapa maisha wachezaji.

Cha ajabu wachezaji wa kigeni wanapata Kila aina ya Msaada wanaotaka na wanasepa wakijiskia ila wa kwetu waawekewa wivu na wapumbavu kama wewe Kwa kutunga upuuzi.

Nzinze kama ana akili awasiliane na Rais vinginevyo nyie wapumbavu mtamharibia future
 
Back
Top Bottom