Acheni mihemko. Yanga ndiyo iliyo muajiri Clement Mzize, na ndiyo yenye haki ya kumuuza kwa bei ambayo wanaona inafaa.
Vipi ikitokea timu ina dau ambalo Yanga wataliridhia? Ni lazima auzwe huko Al Masry? Ni lazima Mzize auzwe kwa dola laki 5, kwa sababu Mayele aliuzwa Pyramid kwa dau hilo?
Siyo kwamba huyo Jasmine ana nongwa? Kwani ni lazima mchezaji mwenye mkataba kuuzwa kwenye timu nyingine inayomhitaji? Alisajiliwa Yanga ili auzwe, au lengo la kwanza ni kucheza mpira na kuiletea timu makombe? Ni kwa nini Yanga isiwe na haki ya kuamua kumuuza mchezaji kwa pesa wanayo ona inafaa, badala ya wakala kuleta mashinikizo yasiyo na tija kwa sababu tu ya 10%?