Yanga yamwekea pingamizi Rais wa TFF Wallace Karia

Yanga yamwekea pingamizi Rais wa TFF Wallace Karia

Natanguliza kwa heri CEO na Eng. Hersi kwenye mpira wa Tz. Siku zenu zinahesabika labda mwamba asirudi kwenye Urais. Kiburi Cha kujiona una sapoti ya wanachama wa Yanga kilimponza Manara na Msemaji wa sasa wa Yanga! Mmoja Mpira ndio basi mwingine aliswekwa ndani. Heshimu Mamlaka.
Kalia naye ni sirikali au kuna wahuni nao wana muunga mkono
 
Mapingamizi yakitupwa na jamaa akichukua Tena kiti?Huyo kawekwa hapo ajajiweka mwenyewe.
Acha kutapeli watu, sio mtu wa sistimu, yeye anajaribu kujifanya kwamba ndio njia ya mitano tena, huku na yeye anapitisha yake.
 
Wanafeli kuhusu nini?

Kama mchezaji anadai, ulitaka Yanga waende ionekane mchezaji hadai??
Mkuu ungesoma kwanza majadiliano tuliojadili na niliye m quote ili upate mantiki ya reply yangu 🙏
 
Linapokuja swala la KISHERIA Yanga huwa wanafeli vibaya sana...... labda kwenye kugoma na kushinikiza lakini sio sheria na kanuni

Hoja ya kwanza.
Kanuni hazijaweka ukomo wa endorsement ila zimeweka minimum...... Yanga walipaswa kuipinga hii kanuni na sio kumshambulia aliyeitumia(ofkoz ni kanuni ya KIHUNI)

Hoja ya pili
Endorsement ni kitendo cha kusaini fomu ya mgombea.... na fomu zimetolewa wakati mmoja.
Yanga wanaweza kuthibitisha vipi kwamba fomu ya Karia ilitolewa mapema na ikawa endorsed kabla ya mchakato wa uchaguzi?

Hoja ya tatu
Vyama vinaendeshwa kwa Sheria na kanuni zilizo sajiliwa na sio SERA
Sheria na kanuni za TFF hazimzuii kugombea
Sasa huko nyuma mjumbe mmoja anaweza kuwaunga mkono wagombea zaidi ya mmoja, lakini kwa sasa mgombea mmoja anaruhusiwa kuunga mkono mgombea mmoja tu! Shida ndiyo ipo hapo jamaa anasema Karia kuaungwa mkono na wajumbe karibu wote wamebaki sijui watatu maana yake wagombea wengine wamekosa endorsement, kwa sababu unatakiwa kupata endorsement zaido ya tano! Hili unalisemeaje?
 
Yanga kama mbabe wa mpira wa Tanzania imedhamiria Kwa dhati kusafisha pale TFF na bodi ya ligi, Sasa nguvu time imehamia Kwa Wallace Karia

CEO wa Yanga Andre Mtine ameandika barua kwenda kamati ya uchaguzi TFF kumwekea pingamizi Wallace Karia

Yanga wameitaka kamati ya uchaguzi TFF kumwondosha Rais Wallace Karia katika mchakato wa uchaguzi wakiwa na hoja kuu 3

1. Matumizi mabaya ya madaraka Kwa kuchukua endorsement 46 kati ya 47.
Sifa ya kukidhinkugombea Urais ni kupata endorsement 5 tu ila Karia amejisanyia endorsement 46 kati ya 47, akijua wazi kufanya hivo ni kuhujumu mchakato wa uchaguzi, maana wagombea wengine watakwama Kwa kukosa endorsement

2 Kuanza kampeni kabla ya wakati.
Karia amekusanya endorsement 46 kabla ya mchakato hii ni dhahiri alizikusanya mapema kabla ya kipenga cha uchaguzi kupulizwa

3 Karia hapaswi kugombea mihula wa mitatu 3
Sera ya michezo nchini imakataza viongozi kukaa madarakani zaidi mihula miwili
Yanga waachane na huu upumbavu. Anachokifanya Karia ndio ambacho ccm wanakifanya kwenye mchakato wa uchaguzi. Injinia Hersi anatarajia yeye na chama chake ccm kushinda ila anasahau wanashinda kwa kudhulumu, sasa tofauti ya ccm na Karia ni ipi!? Wote wanafaidika kwa dhuluma za uchaguzi. Wavumilie tu
 
Akili za Watanzania ni mbovu
Kwaiyo watu kuhoji mifumo mibovu ya dhambi?
Hiyo mifumo mibovu huyo Injinia haioni huko ccm alikochukua fomu kutaka Ubunge!? Hajui akipitishwa na yeye atafaidika na hiyo mifumo mibovu ya uchaguzi!? Ni mpumbavu sana huyo jamaa aisee!
 
Back
Top Bottom