Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee

Bodi ya ligi na TFF walisema sababu za kuhairisha mechi ni uvunjifu wa usalama ambapo watu wenye taaluma za usalama police walikanusha kuwa tarehe 8 March hapakuwa na uvunjifu wa amani

Kuhusu Rushwa, TAKUKURU walikanusha kutambua rushwa yoyote kwenye huo mchezo

TFF wameinyonga Yanga na Karia alionesha kuiunga bodi ya ligi na Simba mkono

TFF waligomea kusikiliza kesi na kuichelewesha maksudi ili kukwamisha Yanga kupata haki Yao ili siku 21 zipite na Yanga asipate haki yake, huu ni uhuni wa wazi wa TFF

Kuna tetesi TFF Kwa mkono wao walijipenyeza CAS na kuishawishi iikandamize Yanga

Sasa TFF kama wanaweza wakaishushe Yanga daraja au waikate points 15 tuone

Huu ni muda wa Yanga kuonyesha ukubwa wake
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
 
Mtakula mlipopeleka mboga. Msomali ana kesi fifa...unawezaje timu Moja kudhamini timu 8 za ligi kuu...hii ndio ubaya ubwela..tuheshimiane kuanzia Sasa. Mtaieleza Dunia kwanini mliinyima timu mnayocheza nayo kutofanya mazoezi uwanja tajwa kama kanuni na Sheria zinavyoelekeza,, na pia mtaiambia Dunia kwanini timu yenu inadhamin timu nane za ligi kuu ambayo inatoa mwanya mkubwa wa upangaji wa matokeo..
 
washushwe daraja kenge hao 😆
 
Haya yanadhihirisha utoto kwenye uongozi wa club ya Yanga.

1.Umeshapewa maelekezo na Mamlaka yajuu ambayo ni CAS ,kwamba nenda kakae na kamati za TFF ukiona umepewa majibu ya kuonewa ndio urudi hapa CAS? Je Yanga hawana iman na CAS!

Undishi wa barua wa kitoto kabisaa,Eti…..kivyovyote,stupid kabisa

Kama hutaki kucheza mechi na Simba unaona utaonewa basi usicheze mechi zote zilizobaki maana zinasimamiwa na TFF 😂😂
 
Hao TFF hawaaminiki ni wahuni tu wana upande wanashabikia kwenye hii kesi

Sasa kama wana uweZo wapange tarehe ya mchezo, waipoke Yanga points 3 na waishishe Yanga daraja wao si wababe
Wacha tuone
 
Tuko pamoja na Yanga Kwa lolote muda wowote
 
Hao TFF hawaaminiki ni wahuni tu wana upande wanashabikia kwenye hii kesi

Sasa kama wana uweZo wapange tarehe ya mchezo, waipoke Yanga points 3 na waishishe Yanga daraja wao si wababe
Wacha
 
Hao TFF hawaaminiki ni wahuni tu wana upande wanashabikia kwenye hii kesi

Sasa kama wana uweZo wapange tarehe ya mchezo, waipoke Yanga points 3 na waishishe Yanga daraja wao si wababe
Wacha tuone
Lakini Ndugu hebu tujadili kidogo?

Yanga hataki kucheza mechi yake na Simba kisa ni Uonevu wa TFF na bodi ya Ligi si ndio? Je uonevu huo ni wa ndani ya uwanja au nje ya uwanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…