Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Yanga alishatoa malalamiko yake mwanzoni kabla ya kwenda huko CAS, swali simple je TFF walimwita Yanga? Yanga alienda CAS sio kwamba hakuwa sababu, bali hakufuata flow kwenye vyombo vya maamuzi sababu tokea siku ile ya kuihirishwa kwa mechi walikuwa hawana imani na TFF pamoja na bodi ya ligi,ndio maana Yanga hakutaka kupitia TFF. Yanga sababu ya kugoma wanayo tena sababu tangible kabisa.

Na ni ngumu sana TFF kutoa maamuzi yatakayo mkandamiza yy mwenyewe, japo yy sio mwenye makosa ila bodi ya ligi chombo kilicho chini yake kina makosa na hakistahili kuwepo mpaka hivi sasa.Ndio maana hata TFF anaogopa kumwita Yanga kuongea nae au kufanya maamuzi sababu maamuzi yoyote yataambatana na nakala. Then hiyo nakala ndio CAS wanaisubiria endapo Yanga asipo ridhika na maamuzi,ndio maana CAS wameirusha Yanga kwa TFF. Hili swala sasa hivi hata yule mwenyekiti wa bodi wameomba busara itumike, walimwita mpaka waziri,sababu kikanuni wanajua washachemka.

Madrid na ukubwa wake alitaka mechi yake isogezwe mbele sababu ya mechi ya marudiano na Arsenal akambiwa utacheza siku iliyo pangwa, juzi akataka kugomea fainal ya Copa Delay sababu ya refa akaambiwa refa habadilishwi. Barcelona baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa alikuwa na mechi 10 mfululizo ana pumzika kila baada ya siku mbili naye kaambiwa hamna mechi itakayo sogezwa mbele na akacheza mechi zote kama zilivyokuwa kwenye ratiba.Al Ahly alitaka refa abadilishwe mechi yake na Zamalek, akakataliwa hakutokea uwanjani Zamalek apewa ushindi wa point tatu na goli tatu. Vyombo vya mpira vinatakiwa viwe na nguvu ya kimaamuzi.Hii incident ingetokea ulaya ni mwendo wa faini, kukatwa point na kampuni zinazo simamia matangazo kudai madai, ila huku kwetu huwaga hatujali kwani tunajua kuna hekima na busara.
 
Lakini Ndugu hebu tujadili kidogo?

Yanga hataki kucheza mechi yake na Simba kisa ni Uonevu wa TFF na bodi ya Ligi si ndio? Je uonevu huo ni wa ndani ya uwanja au nje ya uwanja?
Uonevu upo nje na ndani ya uwanja
Kwanini bodi ya ligi ilihairisha mechi kihuni?
Kwanini Rais wa TFF Karia alionesha wazi yupo upande wa bodi ya ligi na Simba?
Kwanini bodi ya ligi walitoa waraka mapema ya kupanga tarehe ya mchezo bila kusubiria hatua za Yanga kama atarejesha kesi TFF
 
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
View attachment 3325134
Kweli ujinga ni kipaji na UTO wamebarikiwa iko kipaji.

Huna imani na TFF lakini ligi anayoiandaa bado unashiriki huu kama sio uzuzu ni nini.

Ningewaona kweli wanamsimamo kama wakiacha kuingiza na timu uwanjani katika mechi zilizobaki maana wanahisi kuonewa.

Wakati tunawaambia ubaya ubwela hamkuelewa mkaja na kikauli mbiu chenu cha kitaarabu kikafia mbali.
 
Uonevu upo nje na ndani ya uwanja
Kwanini bodi ya ligi ilihairisha mechi kihuni?
Kwanini Rais wa TFF Karia alionesha wazi yupo upande wa bodi ya ligi na Simba?
Kwanini bodi ya ligi walitoa waraka mapema ya kupanga tarehe ya mchezo bila kusubiria hatua za Yanga kama atarejesha kesi TFF

Je uonevu huo utafanywa kwa mechi y simba na yanga pekee?
Maana bado una mechi za kucheza pia ambazo zinasimamiwa na bodi ya Ligi,kwanini usigomee zote
 
Je uonevu huo utafanywa kwa mechi y simba na yanga pekee?
Maana bado una mechi za kucheza pia ambazo zinasimamiwa na bodi ya Ligi,kwanini usigomee zote
TFF kama baba wa mpira Tanzania hapaswi kuonyesha upande

Yanga ananyongwa na TFF ya Karia Toka zamani
 
Hawana imani na Bodi ya ligi halafu wanagomea mechi moja ndio nini?

Msimamo thabiti ilikuwa wagomee ligi yote
 
Haya yanadhihirisha utoto kwenye uongozi wa club ya Yanga.

1.Umeshapewa maelekezo na Mamlaka yajuu ambayo ni CAS ,kwamba nenda kakae na kamati za TFF ukiona umepewa majibu ya kuonewa ndio urudi hapa CAS? Je Yanga hawana iman na CAS!

Undishi wa barua wa kitoto kabisaa,Eti…..kivyovyote,stupid kabisa

Kama hutaki kicheza mechi na Simba unaona utaonewa basi usicheze mechi zote zilizobaki maana zinasimamiwa na TFF 😂😂
Eti hawana imani na TFF wakati hadi bonanza la Muungano linaloandaliwa na hao hao TFF wameenda wakati wangeweza kulisusa bila kuwa na athari yoyote kwao ila wanakuja kususa huku. Hizi siasa tu!

Anyway, Ubaya Ubwelaaaa.
 
Tunaanza na timu ya Rais Karia 5imba
Karia ni shabiki wa Simba anaipendelea 5imba Sasa awape ubingwa huu na aishushe Yanga daraja tuone kama ana huo uweZo mpumbavu yule
 
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
View attachment 3325134
Mnamtisha nani nyie chura
 
Back
Top Bottom