Yanga alishatoa malalamiko yake mwanzoni kabla ya kwenda huko CAS, swali simple je TFF walimwita Yanga? Yanga alienda CAS sio kwamba hakuwa sababu, bali hakufuata flow kwenye vyombo vya maamuzi sababu tokea siku ile ya kuihirishwa kwa mechi walikuwa hawana imani na TFF pamoja na bodi ya ligi,ndio maana Yanga hakutaka kupitia TFF. Yanga sababu ya kugoma wanayo tena sababu tangible kabisa.
Na ni ngumu sana TFF kutoa maamuzi yatakayo mkandamiza au kujikandamiza yy mwenyewe, japo yy sio mwenye makosa ila bodi ya ligi chimbo kilicho chini yake kina makosa na hakistahili kuwepo mpaka hivi sasa.Ndio maana hata TFF anaogopa kumwita Yanga kuongea nae au kufanya maamuzi sababu maamuzi yoyote yataambatana na nakala. Then hiyo nakala ndio CAS wanaisubiria endapo Yanga asipo ridhika na maamuzi,ndio maana CAS wameirusha Yanga kwa TFF. Hili swala sasa hivi hata yule mwenyekiti wa bodi wameomba busara itumike, walimwita mpaka waziri,sababu kikanuni wanajua washachemka.
Madrid na ukubwa wake alitaka mechi yake isogezwe mbele sababu ya mechi ya marudiano na Arsenal akambiwa utacheza siku iliyo pangwa, juzi akataka fainal ya Copa Delay sababu ya refa akaambiwa refa habadilishwi. Barcelona baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa alikuwa na mechi 10 mfululizo ana pumzika siku mbili naye kaambiwa hamna mechi itakayo sogezwa mbele.Al Ahly alitaka refa abadilishwe mechi yake na Zamalek, akakataliwa hakutokea uwanja Zamalek apewa ushindi wa point tatu na goli tatu. Vyombo vya mpira vinatakiwa viwe na nguvu ya kimaamuzi.Hii incident ingetokea ulaya ni mwendo wa faini, kukata point na kampuni zinazo simamia matangazo kudai madai, ila huku kwetu huwaga hatujali kwani tunajua kuna hekima na busara.