vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Jana Yanga wamepoteza dhidi ya Belouizdad kwa kufungwa goli tatu kwa bila. Kimpira, Yanga alicheza soka safi sana na walikuwa wanapiga mipira ya kasi sana ila safu ya ulinzi ikawa inajisahau sana kurudi, magoli wamefungwa ya counter attacks nadhani ni somo kwao ni vitu vidogo sana vilivyowangusha.
Kuna watu wamewachukulia poa Belouizdad ila kama timu ya wazee wangecheza na hawa jamaa pengine ingejirudia ya zama za magoli matano. Jamaa wanajua kuzitumia nafasi chache wanazozipata. Ili Yanga aweze kufuzu ni lazima, tena lazima apate alama tatu dhidi ya Al Ahly kwa Mkapa.
Kwanini fixture ipo upande wa Yanga?
Yanga atacheza mechi yake ya pili dhidi ya Al Ahly, kama atashinda atakuwa na point 3.Mechi mbili zinafuata zote ni dhidi ya Medeama, hapo inatakiwa Yanga apate point zote sita kwa Medeama. Ili imfanye kufikisha point 9 huku akibakisha michezo miwili (mmoja home na mmoja away).
Kwenye michuano ya klabu huwa mara nyingi sana timu zilizopo pot 3 zinasonga mbele hatua inayofuata kwasababu mpangilio wa mechi zinawabeba sana.