Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Ujumbe wa nyota wa zamani wa Barcelona na Man City, Yaya TOURE juu ya uwepo wa fainali mbili kwenye michuano ya Afrika.
Wakati umefika kwa mashabiki wa soka wa nchi zetu barani Afrika kudai HAKI YA MICHEZO kwa kuitaka CAF kuwa na mechi moja pekee ya fainali kwenye uwanja wa usiofungamana na upande wowote (neutral) au fainali mbili kwenye Uwanja wa neutral.
Ni aibu kwa bara letu kuona unyonge wa mchezo bora pendwa wa fainali ya soka duniani (ukitazamwa na mamilioni ya watu duniani) kushuhudia udhalilishaji wa timu ya ugenini kukumbana na mashambulizi ya kuvizia kwa fataki nyakati za usiku wakiwa wamepumzika katika uwanja wao wakiwa hotelini.
Kana kwamba haitoshi, wakati wa mchezo tulishuhudia (vijana waokota mipira (ball boys) wakirusha mipira mingi kwa wakati mmoja ili kupoteza muda kwa ajili ya timu za nyumbani, zaidi ya fataki mbili nzito zilipigwa kiasi cha kupelekea mechi kusimamishwa (mara tatu) ili kuruhusu moshi huo kutoweka, yote haya yalifanywa mbele ya rais wa CAF na ulimwengu mzima wa mashabiki wa soka wakitazama.
Hii sio mara ya kwanza barani Afrika Basi aibu kwenu CAF & FIFA kwa kujua haya yote yatatokea na bila kufanya lolote ila kukaa tu na kutazama onyesho la kupendeza la uharamu na kumtawaza mpiga picha na kombe la ubingwa akiota na kufikiria kuwa hii ingekoma?
Natumai FIFA ingefanya soka kuwa mchezo mzuri tena.