Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

Mashabiki sio wanaocheza mpira. Kipinsi cha CORONA timu zilikuwa zinacheza bila mashabiki na maisha yaliendelea.
Ona huyu, kipindi kile baadhi ya timu ziliwaomba wachezaji wao wapunguze mishahara hali ilikuwa ni teter na hapo ni club kama Barcelona vp hizi zetu za ilala boma fc😀
 
Bora kaongea Yaya ambaye hana maslah na wala haijui Yanga. Baada ya kumaliza maneno yote tupo paleee msimu ujao yakiwatokea majirani tutawakumbusha maneno yao
 
huyo Yaya atulie asitusumbue, hivi Africa timu gani inaweza kwenda na mashabiki ugenini alau 2000? kwa hiyo iyo fainali ikachezwe majukwaa matupu?
 
Motsepe aliwai kuifafanua hii kwamba ikiwa final mechi moja itapigwa uwanja wa neutral mashabiki wengi awana msuli wa pesa,Africa njaa waya mkali mashabiki watashindwa gharama za kukwea pipa,gharama za hoteli n,k

mfano final iwe Yanga Vs Usm Alger alafu mbungi ikapigwe Lagos mashabiki wangapi wataenda Lagos Nigeria kucheki game!
Kwahiyo hizi match 2 ni kwa ajili ya mashabikiii? Basi wanayo haki hao mashabiki kupuliza moshi na kupiga mafatakiiii, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Lakini mpira ilisimama vipindi vyote viwili. Ulivyosimama kipindi cha kwanza, muda uliopotea ulifidiwa kabla ya mapumziko. Dakika 5 sijui 6 zilizoongezwa kipindi cha pili ni fair kwa muda uliopotea kipindi cha pili kwa sababu nadhani haukusimama kwa zaidi ya dakika 2. Kama unashindwa kufunga kwa dakika 90 toka goli la kwanza, kulilia dakika 3 za nyongeza ni kutafuta kisingizio tu.

Kawaida mashindano haya, tegemea timu ya nyumbani kupata favour fulani. Hata Yanga game ya kwanza alipewa dakika 10 za nyongeza. Je alistahili? Na hili nililisema mapema msitegemee nyongeza za namna hiyo kule nikaonekana sina akili.
Kila mtu ashinde kwaooo, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mazingira yetu hasa kiuchumi ni tofauti kabisa na Ulaya, hatuwezi kwenda kwa ndege Afrika Kaskazini, au Magharibi kushangilia timu zetu zikicheza hiyo fainali moja, bado naona patakuwepo na kasoro tu.

Hili kama litatokea, litaleta mgawanyiko, ambapo ikitokea mechi ikachezwa nchi za weusi, inayomhusisha mwarabu na mweusi, basi wale mashabiki wa nchi husika automatically watajikuta wakimshangilia mweusi mwenzao dhidi ya mwarabu, na vice versa.

CAF nao wanavyopendelea waarabu, wanaweza kusingizia waarabu ndio wenye viwanja vizuri, basi fainali nyingi zikawa zinachezwa Arabuni.

Hapa sioni kama CAF wanalakufanya, hawana ujanja, lazima watulie na mfumo huu uliopo kila mmoja ajue namna ya kutumia uwanja wake wa nyumbani, akiwa na mashabiki wake, kupata ushindi mnono utakaomuwezesha kushinda kombe.
 
Kawaida ya waswahili hua ni kulalamika baada ya Sheria kuwakata, hata kama fainali ingekua moja yanga angepoteza tuu,

lakini kubwa zaidi Africa bado haijawa tayali kwa fainali moja kwa sababu ya mashabiki kwanza wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za kwenda kutazama timu zao zikienda kucheza mbali na nchi zao au karibu kutokana na vipato vyao kua vidogo,

Na hata ikiotokea fainali ikawa moja na walivyo jaribu hapo nyuma kidogo alafu hiyo mechi ikachezwa kwenye nchi ambayo haijatoa mwana fainali, ni ngumu Sana kwa hiyo mechi kupata mashabiki wengi mfano mzuri ni kwenye Afcon, mwenyeji akitoka mapema tuu na Mashabiki uwanjani wanapungua kabisa

Bora fainali zibaki kua mbili hivyo hivyo
 
Nina MASHAKA na source ya Hiyo habari.

Nimejaribu KUMUULIZA Kitenge amejibu heeeee si unajua Tena.......

SIDHANI KAMA NI HABARI YA KWELI.
habari ya kweli inafafanaje, wapumbavu km wewe ndio mnafurahia huo upuuzi. Hovyo kabisa, ulitegemea source ya itoke wapi. Hata km ni nani angeandika ni ujumbe murua uliokuja kwa wakati sahihi
 
UJUMBE wa nyota wa zamani wa Barcelona na Man City, Yaya TOURE juu ya uwepo wa fainali mbili kwenye michuano ya Afrika.

✍️ Wakati umefika kwa mashabiki wa soka wa nchi zetu barani Afrika kudai HAKI YA MICHEZO kwa kuitaka CAF kuwa na mechi moja pekee ya fainali kwenye uwanja wa usiofungamana na upande wowote (neutral) au fainali mbili kwenye Uwanja wa neutral.

Ni aibu kwa bara letu kuona unyonge wa mchezo bora pendwa wa fainali ya soka duniani (ukitazamwa na mamilioni ya watu duniani) kushuhudia udhalilishaji wa timu ya ugenini kukumbana na mashambulizi ya kuvizia kwa fataki nyakati za usiku wakiwa wamepumzika katika uwanja wao wakiwa hotelini.

Kana kwamba haitoshi, wakati wa mchezo tulishuhudia (vijana waokota mipira (ball boys) wakirusha mipira mingi kwa wakati mmoja ili kupoteza muda kwa ajili ya timu za nyumbani, zaidi ya fataki mbili nzito zilipigwa kiasi cha kupelekea mechi kusimamishwa (mara tatu) ili kuruhusu moshi huo kutoweka, yote haya yalifanywa mbele ya rais wa CAF na ulimwengu mzima wa mashabiki wa soka wakitazama.

Hii sio mara ya kwanza barani Afrika Basi aibu kwenu CAF & FIFA kwa kujua haya yote yatatokea na bila kufanya lolote ila kukaa tu na kutazama onyesho la kupendeza la uharamu na kumtawaza mpiga picha na kombe la ubingwa akiota na kufikiria kuwa hii ingekoma?

Natumai FIFA ingefanya soka kuwa mchezo mzuri tena.

#KitengeSports
FB_IMG_1685969021847.jpg
 
Back
Top Bottom