Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

On my side......
Nafikiri ifikie hatua africa tukubaliane kuwa huu ndio mchezo wetu. Mashabiki wa soka hususani Tanzania wasifananishe soka la africa na ulaya.
Wajapo waarabu ni muhimu kuwalaza kwenye mabangaloo morogoro au Tanga isiwe mbali sana na dar. Wale ugali kwa kabeji.. uwanjani waletwe kwa gari kisha kila shabiki na wachezaji asisahau bisibisi ama nondo ndogo ndogo.. teknolojia ya mafataki ni muhimu kwetu hasa hasa timu inapo lemewa. Tukifika hatua hii hakika soka la Africa litakuwa bora na la kupendeza hata msumbiji watafika robo fainali
 
Kwahiyo ile game mliipoteza kwasababu ya dakika? Ile game hamukuwa na uwezo wa kufunga tena, plan yenu ya kushambulia ilikuwa imebanwa tayari ndiomaana ilifikia hatua kocha akaamua kujaribu bahati kwa kufanya sub holela.

Bila ile penalty sidhani kama kungekuwa na lolote la maana.
zero shot on target FC siwezi kuongea na wewe
 
Me hata ligi ya bongo nimeacha rasmi ni ujinga na uhuni na upangaji matokeo tu.Hakuna ligi ni ujinga
kabsa yani ni Ligi za kitoto sana yan watu wanauza mechi had mashabki tunaon kabsa, kiukwel mi naach kuangalia haya mashudu ya Afrika acha nibaki na Liverpool na Napoli Tu.
 
Hata ingekuwa fainali moja shughuli ilishaisha kwa mkapa.2-1.
 
Motsepe aliwai kuifafanua hii kwamba ikiwa final mechi moja itapigwa uwanja wa neutral mashabiki wengi awana msuli wa pesa,Africa njaa waya mkali mashabiki watashindwa gharama za kukwea pipa,gharama za hoteli n,k

mfano final iwe Yanga Vs Usm Alger alafu mbungi ikapigwe Lagos mashabiki wangapi wataenda Lagos Nigeria kucheki game!
Zibakie mbili tu ili kila timu ifaidi 'home advantage'.
 
Utopolo wahed , kuingia fainali moja tuu ya kombe la loosers na kupoteza kizembe kabisa kutokana na makosa ya kiafrica wanataka kuipangia CAF sheria ya fainali

Last season fainali ilikua mechi moja kati ya mabingwa Waydad dhidi ya AlAhly pale Morroco

Fainali ilipoisha msimu huu wakaona warudi tuu kwenye fainali mbili ( maoni ya ma Giant wa Africa) na wao wanaona ni sawa tuu

Sasa ninyi wala mihogo baada ya kufungwa mnatafuta kuchaka cha kujifichia
 
View attachment 2646558

Ujumbe wa nyota wa zamani wa Barcelona na Man City, Yaya TOURE juu ya uwepo wa fainali mbili kwenye michuano ya Afrika.

Wakati umefika kwa mashabiki wa soka wa nchi zetu barani Afrika kudai HAKI YA MICHEZO kwa kuitaka CAF kuwa na mechi moja pekee ya fainali kwenye uwanja wa usiofungamana na upande wowote (neutral) au fainali mbili kwenye Uwanja wa neutral.

Ni aibu kwa bara letu kuona unyonge wa mchezo bora pendwa wa fainali ya soka duniani (ukitazamwa na mamilioni ya watu duniani) kushuhudia udhalilishaji wa timu ya ugenini kukumbana na mashambulizi ya kuvizia kwa fataki nyakati za usiku wakiwa wamepumzika katika uwanja wao wakiwa hotelini.

Kana kwamba haitoshi, wakati wa mchezo tulishuhudia (vijana waokota mipira (ball boys) wakirusha mipira mingi kwa wakati mmoja ili kupoteza muda kwa ajili ya timu za nyumbani, zaidi ya fataki mbili nzito zilipigwa kiasi cha kupelekea mechi kusimamishwa (mara tatu) ili kuruhusu moshi huo kutoweka, yote haya yalifanywa mbele ya rais wa CAF na ulimwengu mzima wa mashabiki wa soka wakitazama.

Hii sio mara ya kwanza barani Afrika Basi aibu kwenu CAF & FIFA kwa kujua haya yote yatatokea na bila kufanya lolote ila kukaa tu na kutazama onyesho la kupendeza la uharamu na kumtawaza mpiga picha na kombe la ubingwa akiota na kufikiria kuwa hii ingekoma?

Natumai FIFA ingefanya soka kuwa mchezo mzuri tena.
CAF walifanya hivyo msimu wa 2020, 2021 na 2022 lakini waliona viwanja vilikuwa havipati mashabiki.

Kumbuka logistics za kusafiri kwa mashabiki katika nchi nyingi za Africa ni changamoto sana. Kufika West Africa na North Africa lazima uende Asia kwanza ndiyo Urudi Africa hata katika nchi za COSAFA lazima ufike South Africa kwanza ndiyo uweze kufikia nchi hizo zingine.

Kingine travel documents kwa Africa bado sana kulinganisha na nchi za Europe ambapo wako kwenye EU hakuna mahitaji ya Visa na mambo mengine.
 
Ilitakiwa vikifanyika vitendo vya makusudi kama tulivyoshuhudia wakifanyiwa, waliofanyiwa vitimbi wapewe ushindi papo hapo kabla hata ya nechi kuchezwa au kumalizika.
Mnataka ushindi wa mezani ?
 
Motsepe aliwai kuifafanua hii kwamba ikiwa final mechi moja itapigwa uwanja wa neutral mashabiki wengi awana msuli wa pesa,Africa njaa waya mkali mashabiki watashindwa gharama za kukwea pipa,gharama za hoteli n,k

mfano final iwe Yanga Vs Usm Alger alafu mbungi ikapigwe Lagos mashabiki wangapi wataenda Lagos Nigeria kucheki game!
Mama Samia atatoa ndege mbili.
 
Lakini mpira ilisimama vipindi vyote viwili. Ulivyosimama kipindi cha kwanza, muda uliopotea ulifidiwa kabla ya mapumziko. Dakika 5 sijui 6 zilizoongezwa kipindi cha pili ni fair kwa muda uliopotea kipindi cha pili kwa sababu nadhani haukusimama kwa zaidi ya dakika 2. Kama unashindwa kufunga kwa dakika 90 toka goli la kwanza, kulilia dakika 3 za nyongeza ni kutafuta kisingizio tu.

Kawaida mashindano haya, tegemea timu ya nyumbani kupata favour fulani. Hata Yanga game ya kwanza alipewa dakika 10 za nyongeza. Je alistahili? Na hili nililisema mapema msitegemee nyongeza za namna hiyo kule nikaonekana sina akili.
Sawa mchambuzi JEMEDARI wetu, tumekusikia.
 
Back
Top Bottom