Sasa na wewe uliwahi kuona lini hasa Israel amewahi kuigwaya Iran? Huyu huyu Israel amekua anajipigia Iran anavotaka? Kaua watalaamu wake wa nuclear kwenye ardhi ya nyumbani, kaua viongozi wa Hamas na Hezbollah ndani ya ardhi ya Iran, kaua rais na waziri wa mambo ya nje wa Iran juzi tu hapo; kaangamiza mitambo yake ya kivita tena, tena this time Israel alitumia matoto ya kike mazuri halafu yana shepu, Iran kabaki hajui afanyaje. Yaani Israel amuogope Iran? Hi nayo sio kweli. I think Israel atamuogopa tu Iran akisikia Urusi atatoa back up but not himself alone
Mkuu huwa nakuamini kwasababu huwa unaelezaga mambo ya hakika na sio udaku.
1)Kufanya assassination attempt ni jambo ambalo sio rahisi mtu kuzuia.
Hao Hamas mara kibao huingia Israel na kuua askari wa Israel na kutoroka na mara nyingi hawakamatwi.
2)Rais wa Iran hajauliwa na Israel hili lilishazungumzwa usiongope kaka.
3)Shambulio lililofanywa na Israel dhidi ya Iran lina limited damage,yani madhara ni madogo kuliko ukubwa wa shambulio,tena hata satellite image zilizoletwa vyombo vya habari ikiwemo BBC vinasema havioneshi vivid evidence ya shambulizi.
Inamaana shambulio ni failure.
Twende kwenye mada kwanini Israel amuogope Iran.
1)2006 aliyeisaidia Hizbollah kumtembezea kichapo Israel pale Jubeir ni Iran,inamaana pasi na Iran kumuunga mkono Hizbollah ingekua ngumu kumsukuma Israel nje ya Lebanon.
2)Vita ya Yemen kuanzia 2013-2021 mfadhili wa Houthi ambayo ilikua inapigana na nchi kamili Saudi arabia na vikundi kama Al qaeda ni Iran.
Aliyefanya Houthi ikasimama na kushinda ni Iran.
3)Aliyeifadhili Houthi kuiteka red sea ukanda wa Baab Al mandib ni Iran.
Unadhani ile meli ya Israel ilitekwa kiwepesi kama sio kwa msaada wa Iran ndani ya Houthi!?
4)Embu tukumbushie retaliation ya Iran dhidi ya Israel kwa mashambulizi ya Promise 1 April na Promise 2 October 1,kila mtu aliona miji ya Israel ikichomeka moto kwa mashambulizi ya makombora ya Iran ndani ya Israel,sio kama shambulizi la kitoto na kipropaganda la Israel ambalo HAKUNA USHAHIDI WA UHARIBIFU ULIOTOKA.
5)Tuje kwa Hizbollah ambao wamerusha makombora Kaskazini mwa Israel na kuwafanya wakaazi zaidi ya laki tatu wahame Kaskazini na kuhamia kanda ya kati na kusini,silaha walizotumia ni Iranian made.
Kipindi Iran ina base pale Syria kabla ya Assad kuanguka Israel hajawahi kukiuka makubaliano ya buffer zone na kujitanua zaidi pale Gollan,ila baada ya Assad kuenguliwa na Iran kuondoa majeshi Israel akapata upenyo.
Tena akiongezea kuwa new regime ikitaka uhasama uongezeke basi iruhusu Iran iwe na uhusiano wa kidiplomasia na wao.
Ili wawe marafiki wasiwe na urafiki na Iran,je hapo hamuogopi?
Hapo bado unataka kusema Israel hamuogopi Iran!???
Mkuu umeongea kiwepesi sana aisee kiasi mengi ni factless nisamehe kama nimekosea kusema hilo.