Yericko Nyerere adai kuingiza zaidi ya Tsh milioni 220 kwa kuuza vitabu Amazon

Inawezekana ni kweli maana anauza kwa bei ya juu sana. Hata kibongobongo alikua anauza 80k kitabu kimoja.

Akiuza nakala 100 tayari ana 8M


Kuna kitabu kingine alikua anauza 1.7M kama sikosei. Sasa hiko akiuza nakala kumi tu yupo mbali.


Uandishi wa vitabu unaweza kukulipa inategemea na aina ya vitabu unavyoandika, promotion unayofanya na price yake iwe ya juu sio unaandika kitabu unauza nakala moja 2000/= na watanzania tusivyopenda kusoma vitabu hadi upate milioni 1 inabidi uuze vitabu 500. Utawapata wapi watu wote hao?

Nipo kwenye hatua ya uandishi wa kitabu nafikiri kitavutia wengi na nitakifanyia branding ya kutosha. Nitakiuza elfu kumi per copy ili kufikia lengo la kuuza nakala 500 nipate zangu milioni tano niingie kuwekeza shambani huko.
 
Kwani hicho kitabu kiliwekwa Amazon kiliandikwa kwa kiingereza?,if not wanunuzi wa kufikisha hiyo hela walitoka wapi?,:acheni kutulisha matango pori kwa data za kupika
Wazungu wako busy sana kwenye kujifunza kiswahili tofauti na wewe uliyeng'ang'ana na kigagagigikoko chako.
 
Mimi nimefurahi juhudi zake zinamlipa.

Jamaa anapambaba sana kukitangaza kitabu chake mitandaoni.

Kuandika kitabu ni jambo moja ambalo ni gumu, kukitangaza kitabu chako angalu kimoja sokoni ni jambo jingine gumu zaidi kuliko kuandika vitabu vinne.

Mara ngapi umeona hapa amekuja na thread nyingi na mwisho anakushauri kasome zaidi kitabu chacke?

Hongera kwake.
 
Yaani kutoka kuwa mpiga ripu wa mtaani mpaka kujenga ghorofa tatu ni maendeleo makubwa sana,nisichoamini ni vipi kitabu cha kiswahili kiuzwe amazoni hadi kufikia hiyo pesa,
 
Ha ha ha,niliwahi andika finction ya kimombo,baada ya kuona soko halieleweki nimeishia chapter 12 nikaona napoteza mda,ngoja nimtafute Brad Thor nimuuzie hili pagale afanye finishing,labda ntalamba hata milioni 100,
lakini nimshauri tu yerico kutotangaza hizi figure maana hazibalance,ufanye biashara ya milioni 200,halafu ujenge ghorofa la bilioni moja ndani ya interval ya miaka 5,
kuna kaharufu ka money laundry
 

Sasa tutaaminije wakati sehemu iliyoandikwa kiasi umefuta?
 
Kwani Lemubebez kile chake ameuza copy ngapi
 
Acheni fiksi..
Hapa I SMELL MONEY LAUNDERING kwa mgongo wa kitabu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…