GE2025 Yericko Nyerere: Mbowe alienda kumuona Lissu gerezani zaidi ya mara tatu

GE2025 Yericko Nyerere: Mbowe alienda kumuona Lissu gerezani zaidi ya mara tatu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu

Yericko Yohanesy Msambila Mkana Nyerere, mwanachama wa CHAUMMA, anasema Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alienda mara tatu gerezani kumuona Mwenyekiti wa sasa, Tundu Lissu.

Je, alikuwa anaenda kumshawishi Lissu alegeze kamba?

 
Wako CHAUMMA ilakila neno ni kuhusu Chadema, baada ya uchaguzi kuisha watakuwa kimya zaidi kwasababu hama yao si kwaajili ya kujenga chama cha CHAUMMA ila kupata nafasi ya kugombea ubunge tu.
 
Hichi chama Cha chauma sijaelewa sera zake ni zipi maana kila mwanachama wake anapoongea anaizumgumzia chadema utafikiri chadema ndio IPO mamlakani Sasa sijui chadema ndio sera yao watakayopeleka kwa wananchi ili wachaguliwe?
 
Wakuu

Yericko Yohanesy Msambila Mkana Nyerere, mwanachama wa CHAUMMA, anasema Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alienda mara tatu gerezani kumuona Mwenyekiti wa sasa, Tundu Lissu.

View attachment 3438245
So what!
20250729_010133.jpg
 
Anatumwa na mtandao kwendakumlainisha mwamba .....amegoma
Asipoenda, kwa nini hajaenda? Hajakubali matokeo ya uchaguzi. Akienda, ametumwa na mtandao. Mtakuwa hivyo hivyo akijitokeza Mahakamani kusikiliza kesi ya Lissu. Uchaguzi uliisha Januari na mlishinda. Yote haya ya nini?

Amandla....
 
Hivi Hawa CHAUMMA wanapambana na CHADEMA ama CCM? Maana ni kama hawajui kama wao siyo tena ni wanachama wa CHADEMA!!
Kwa hiyo asijibu swali kwa sababu linahusu Chadema? Na akijibu asiseme ukweli wake ili kukisitiri Chadema? Sasa hivi Chadema na Chaumma ni vyama vinavyo shindana. Kwa mtazamo wa Chaumma, CDM haikuwatendea haki na bado wanaendelea kuwafuata fuata.

Amandla...
 
Anatumwa na mtandao kwendakumlainisha mwamba .....amegoma
Ninyi vijana wa Chadema hamjawahi kuwa akili timamu. Asingeenda mngemsema kwanini haendi. Ameenda mnamsema kwanini ameenda! Ila uzuri wenu mnajiita akili kubwa! Ahahahahaha!!
 
Back
Top Bottom