YESU aliyezaliwa, hana baba wala mama, Ni Mungu aliyekuja Katika mwili wa mwanadamu


NAWATAHADHARISHA NDUGU ZANGU...
Msiendelee kudhalilisha ukuu wa Mungu, mtakuja kuangamia kwa kukosa maarifa...
Yaani hata kwa akili ya kawaida
Kiumbe chenye sifa zifuatazo ni dhaifu sana na hakistahili hata kidogo kulinganishwa na Mungu mmoja na mwenye mamlaka yote

1. Mungu gani anakwenda choo kama sisi
2. Mungu gani anakula ugali na mikate kama sisi
3. Mungu gani anaugua kama sisi
4. Mungu gani analala usingizi kama sisi
5. Mungu gani anakesha akimuomba Mungu kama sisi
6. Mungu gani anakufa ili awasamehe walio mkosea?

KUMUITA YESU KUWA NI MUNGU NI KUDHALILISHA UKUU WA MUNGU, KWA BAHATI NZURI ALISHA TUONYA KUWA; WATU WENGI WATAKUJA KUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA!

Hapa ndio hupata wasiwasi na baadhi ya vifungu kama kina Isaya kama kweli vimetoka kwenye reliable source....
 
Rudia kusoma Isaya 9:6

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume,
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake,

Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu,

Mungu mwenye nguvu ,

Baba wa milele,

Mfalme wa Amani,

7: Na Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe.

... mwisho wa kunukuu...


Kwa fikra zako huyo aliyezaliwa aitweje Baba wa milele?

Na ufalme wake uwe hauna mwisho?

YESU ni MUNGU aliyekuja Katika mwili wa mwanadamu.

Amini uokoke, au mkatae uangamie,

Alikuja kwa watu wote maana ndiye alliyewaumba na kuwapa pumzi hai WEWE ukiwamo.

Karibu Katika ufalme wa Mungu.

Aamin
 
Isaya 9:6
Aliyezaliwa ni baba wa milele.

Nimequote neno la Mungu.

Sasa ni uamuzi wako kuamini au kuwa mpinga Kristo.

Mungu ni mmoja tu, na jinale ni YESU Kristo/Yeshua Hamashiach
NABII ISAYA ALIKUWA DINI GANI?
 
Nipo na wana hapa tunakula gambe ingawa sina uzoefu nayo..

Kwahiyo yethuu alizaliwa bila dingi wala maza au sijaelewa nimelewa?
Ndio hivyo,

Yusuph SI biological father wa YESU,

Wala Mary sio biological mother wa YESU,

Ingekuwa Leo, ungechukua DNA yake, ingeleta utata, sababu YESU ni MUNGU aliyekuja Katika mwili wa mwanadamu.

Hata walevi huwa tunawahubiria bila shida maana pombe huingia tumboni na ubongoni, SI Katika akili iliyo Katika nafasi na roho.
 
Leta ushaidi mm sio mjinga mpaka niamini maneno matupu
Ushahidi ni neno la Mungu.

Nimequote hapo kuzaliwa kwa YESU Me Mathew 1 nzima na chapter 2.

Ipo wazi kuwa Yusuph hakuwa biological father wa YESU,

ISAIAH 9:6

Inasema bikra atachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume,

Ambaye ni

1. Mfalme wa Amani

2. Mungu mwenye nguvu.

3. Mshauri wa ajabu

4. Baba wa milele

5. Na ufalme wake hauna mwisho, ni wa milele.

Sasa unataka ushahidi upi ikiwa maandiko yako wazi kuwa mtoto huyo ni 2. Mungu mwenye nguvu?

Mungu akupe kuelewa na uamini, Ili upofu ukuondoke.
 
Nipo na wana hapa tunakula gambe ingawa sina uzoefu nayo..

Kwahiyo yethuu alizaliwa bila dingi wala maza au sijaelewa nimelewa?
Kupitia Roho Mtakatifu

Luka 1: 31
Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

Luka 1:35
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
 
Kama hakuna ushaid ni utapel kama utapel mwingne
Ushahidi upo hata sasa,

Huyu Mungu aliyekuja Katika mwili wa mwanadamu,

1. Alizaliwa,

2. Akafa( mwili),

3. Akafufuka na kupaa mbinguni.

Nenda Israel hata Leo, kaburi alozikiwa lipo, ila mifupa ya alozikwa haipo sababu alifufuka na kupaa mbinguni.

Neno la Mungu limethibitishwa.

Amini uokoke.

Aamin
 
Empty tomb alozikiwa ipo Israel hata sasa aende,

Ikiwa hataki kuamini picha,

Aende akajiridhishe mwenyewe pale Israel kwa Gharama zake.
Kabisa

Kuachana na hayo pia kuna mambo mengine mazito au knowledge
Kwenye high dimensions ambazo
Mtu kwenye low dimension anaweza akaona ni ukichaa lakini yule anayeoperate huko anahitaji aamini zaidi ili apate siri zaidi zilizofichwa
.
 
Kabisa

Kuachana na hayo pia kuna mambo mengine mazito au knowledge
Kwenye high dimensions ambazo
Mtu kwenye low dimension anaweza akaona ni ukichaa lakini yule anayeoperate huko anahitaji aamini zaidi ili apate siri zaidi zilizofichwa
.
Ni kweli.

Imani muhimu,

Na chanzo Cha Imani ni kusikia.

Nimemfanya asikie, ndipo aamini.

Na kutokuamini ni dhambi, aamini Ili aepuke hukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…