Salaam ,shalom!
Hii ni habari njema!!
GOOD NEWS😅💥🔥🎉🎊
Asomaye na afahamu,
Imeandikwa zamani vitabu vya unabii kuwa YESU ni mwana wa Daudi.
Pia ukisoma kuzaliwa kwa YESU Mathayo chapter 1, ukoo wa YESU umeanzia huko Kwa Daudi, Mwana wa Ibrahim.
Mathew 1:16.
Yakobo akamzaa Yusuph mumeweMariam aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Mathew 1:18
Kuzaliwa kwake YESU Kristo kulikuwa hivi. Mariam mama yake alipokuwa ameposwa na Yusuph, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho mtakatifu.
Yusuph akadhamiria kumwacha, ila malaika akamtokea ndotoni kukwambia asimwache amlee.
Somo hapo ni kuwa, Mungu alikuja mwenyewe Katika mwili wa mwanadamu kwa kazi maalum ya ukombozi.
Na kwa kuwa, Yusuph hakuhusika Katika kupatikana kwa YESU, anakuwa baba mlezi tu,
Na Mary kwa kuwa alikuwa Bikra kabla ya kupata ujauzito na baada ya ujauzito, pia SI mama wa YESU, ni mama mlezi tu kama alivyo Yusuph. (Isaya 7:14),( Mathew 1:23)
YESU NI MUNGU AJE.
(Isaya 9:6-7)
6: Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume,
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa JINA lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa Amani.
7: Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti Cha enzi Cha Daudi na Ufalme wake,
Kuuthibitisha na kuutegemeza,
Kwa hukumu na kwa haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
...Mwisho wa kunukuu...
Yaani kumbe YESU ndiye Mungu Baba Katika roho ( Isaya 9:6), ndiye aliyekuja Katika mwili wa mwanadamu.
Hii ni Siri kubwa.
Ikiwa hujampa YESU Kristo maisha yako, fuatisha salaam hii:
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO,NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA,NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU ISINISHINDE, UZINZI USINISHINDE,NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AAMIN