Yeyote aliyeajiriwa na anataka kujiajiri; anza kununua vitendea kazi kwa ajili ya ajira yako mpya

Yeyote aliyeajiriwa na anataka kujiajiri; anza kununua vitendea kazi kwa ajili ya ajira yako mpya

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kumiliki vitendea kazi muhimu, ni rahisi kuacha kazi na kwenda kujiajiri. Wengi tunashindwa kufikia hayo malengo, kwa sababu mishahara yetu tunatumia kwenye vitu vinavyokula hela na havizalishi.

Utakuta mtu anachukua mkopo mkubwa au anatumia fedha alizopata kwenye ajira kwa kujengea nyumba, kununua magari ya starehe, au kutumia kwenye anasa zingine n.k; huyu mtu ni vigumu kuja kujiajiri. Kama atajiajiri, labda awe ameachishwa kazi.

Kwa yeyote mwenye vimelea vya kujiajiri, matumizi yake ya fedha huwa ni kununua mashine mbalimbali kama:​
  • Mashine za kusaga nafaka n.k​
  • Mashine za kutengeneza vinywaji​
  • Mashine za ushonaji​
  • Mashine za kuchapa nguo​
  • Mashine za kutengeneza magari​
  • Mashine za kushona mabegi, viatu n.k​
  • Mashine za mbao n.k​
  • Mashine za kuchakata ngozi n.k​
Kwa ujumla, fedha zake atatumia kwenye kununua kitu kitakacho mzalishia bidhaa na kuipeleka sokoni, na hatimaye kupata fedha.

Huyu ana nafasi kubwa sana kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa.​
 
Mleta mada umetusaidia sana. Hiyo ni akili ya ujasiriamali, watu wanaokaribia kustaafu (na hata sisi wengine), jamaa ametupatia desa hilo.
 
Mtu amemaliza chuo almanusura aache chuo sababu ya msosi vp huo mtaji anautoa wapi au wewe unaongelea wastaafu.
 
Mtu amemaliza chuo almanusura aache chuo sababu ya msosi vp huo mtaji anautoa wapi au wewe unaongelea wastaafu.
Upatapo ajira, yale mapato unawekeza kwenye vitendea kazi
 
Umenikumbusha mbali, nakumbuka kuna rafiki yangu ambae alikua anatushangaza sana, tulipoanza kazi wengi tulianza kwa kununua vitu vya ndani yeye alikua bz kununua misumeno,randa,patasi yani vifaa vya useremala kwa ujumla, na cha ajabu ajira yetu haikua na uhusiano wowote na useremala, baadae alifungua karakana ndogo ya useremala na baada ya miaka miwili aliachana na ajira na hivi sasa ni tajiri mkubwa kwenye maswala ya fanicha na maduka ya hardware.
 
Aliona mbali mkuu
 
Umezungumzia jambo zuri sana, Je hizi mashine baadhiyake nazipatia sehemu gani Tanzania, Mashine ya kusaga na mashine ya kushona mabegi....

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom