Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kumiliki vitendea kazi muhimu, ni rahisi kuacha kazi na kwenda kujiajiri. Wengi tunashindwa kufikia hayo malengo, kwa sababu mishahara yetu tunatumia kwenye vitu vinavyokula hela na havizalishi.
Utakuta mtu anachukua mkopo mkubwa au anatumia fedha alizopata kwenye ajira kwa kujengea nyumba, kununua magari ya starehe, au kutumia kwenye anasa zingine n.k; huyu mtu ni vigumu kuja kujiajiri. Kama atajiajiri, labda awe ameachishwa kazi.
Kwa yeyote mwenye vimelea vya kujiajiri, matumizi yake ya fedha huwa ni kununua mashine mbalimbali kama:

- Mashine za kusaga nafaka n.k
- Mashine za kutengeneza vinywaji
- Mashine za ushonaji
- Mashine za kuchapa nguo
- Mashine za kutengeneza magari
- Mashine za kushona mabegi, viatu n.k
- Mashine za mbao n.k
- Mashine za kuchakata ngozi n.k
Kwa ujumla, fedha zake atatumia kwenye kununua kitu kitakacho mzalishia bidhaa na kuipeleka sokoni, na hatimaye kupata fedha.
Huyu ana nafasi kubwa sana kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa.
Huyu ana nafasi kubwa sana kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa.