Yeyote Anayetaja Amani Bila Kutaja HAKI, Ni Mnafiki, Tumzomee.

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Kuitafuta haki kwa anayeonewa na kunyimwa haki yake, ni tendo halali na takatifu, na ni wajibu wa msingi.

Siku hizi wadhulumaji wa haki za wananchi , ili waendelee kudhulumu haki za wananchi, wanajificha nyuma ya neno amani, lakini hawathubutu kutaja HAKI.

Amani ni zao la HAKI, huwezi kuitaja amani bila HAKI, halafu ujifanye wewe eti ni mpenda amani. Unafanya matendo ya kuwanyima watu HAKI zao, mdomoni unaropoka neno amani, halafu utegemee kuna wajinga watakuona wewe ni mpenda amani. Yeyote anayedhulumu haki za wananchi, ni mvurugaji mkubwa na shetani mkubwa dhidi ya amani ya Taifa.

Ukiona mtu amekazania kutaja tu amani, lakini anaogopa kuitaja haki, tambua kuwa mtu huyo ni mnafiki, mwongo na pengine ndiye mhatarishaji mkubwa wa amani ya nchi, kutokana na matendo yake ya dhuluma kwa wananchi.

WITO MKUU
Kila wananchi ana wajibu wa kuitafuta, kuilinda na kuipigania haki. Wananchi wawatambue wadhulumaji wa haki kutokana na matendo na kauli zao. Wananchi wawatambue na kuwakataa watu wanafiki, waongo, wanaopalilia uharibifu wa amani kwa kudhulumu haki, watu wanaowadharau wananchi na kuwaona ni wajinga wasio na akili, wasioweza kuona matendo ya dhuluma dhidi ya haki, wanayofanyiwa.

kuanzia sasa, ni vema akitokea mtu mnafiki na mwongo, akataja amani, kabla ya kutaja HAKI, Wananchi tupige kelele kwa kuitikia HAKI HAKI HAKI, TUNAITAKA HAKI.
 
Wanajijua hadi mioyo yao
 
CCM ni wataalamu wa kujizima data
 
Kwa sasa neno haki limeanza kushika nguvu dhidi ya hadaa ya muda mrefu ya amani. Muda mrefu amani imetumika kama kitisho cha kudai haki. Ila kizazi hiki sasa kimejua kina wajibu wa kupigania haki, kwani amani automaticaly itakuja kukiwa na haki.
 
huo ni upotoshaji wa wazi kabisa gentleman,
haki inaambatana na wajibu, vinginevo ni fujo na usumbufu kwa wasiohusika na haki yako
 
huo ni upotoshaji wa wazi kabisa gentleman,
haki inaambatana na wajibu, vinginevo ni fujo na usumbufu kwa wasiohusika na haki yako

Sentensi yako ni sahihi lakini umeiweka hovyo kutetea uwongo.

Nakutolea mfano mdogo:
Nikilipa kodi, natimiza wajibu wangu, kwa kuwa nimetimiza wajibu wangu wa kulipa kodi, kupata huduma toka mamlaka mbalimbali zinazoendeshwa na kodi yangu, ni haki yangu. Nikipewa haki yangu ya huduma, ninakuwa na amani moyoni.

Lakini kuna haki za msingi zinazoelekezwa na katiba au sheria mbalimbali:
Kwa mfano mwananchi ana haki ya kushiriki kwenye uchaguzi ili kumchagua kiongozi anayefaa, lakini ni kwenye uchaguzi ulio wa haki na huru. Hapo kuna mambo ya msingi:
1) Haki ya mwananchi kuchagua kiongozi
2) Mifumo ya uchaguzi inayowezesha uchaguzi ulio huru na wa haki.

Mwananchi akiona lolote katika hayo mawili linaporwa na yeyote, ni lazima ayapiganie, ni wajibu wake wa kikatiba, kwani kila mwananchi anatakiwa kuilinda katiba dhidi ya waharibifu wake.

Mfano wa pili, katiba yetu inatamka wazi kuwa Mahakama ni muhimili unaotakiwa kuwa huru, usioingiliwa na muhimili mwingine wowote. Polisi kwenda mahakamani na kuteka watu na kuwaumiza, ni ukiukaji mkubwa wa katiba yetu. Mamlaka yote kwa masuala yanayohusu mahakama, yapo chini ya muhimili wa mahakama, siyo polisi. Kama kuna mazingira ambayo maagizo ya mahakama yamekataliwa na yeyote, na mhusika hataki kuitii mahakama, hapo mahakama inawezs kuomba usaidizi kutoka vyombo vya dola, na vyombo vya dola vitalazimika kufanya kazi kwa kuzingatia maombi ya mahakama.

Kilichofanywa juzi na polisi ni ushenzi wa hali ya juu dhidi ya katiba yetu na dhidi ya uhuru wa mahakama. Na wananchi kukemea jambo hili na kuhakikisha halitokei tena, ni wajibu wa kila mwananchi aliye mkweli na ambaye siyo mnafiki.

Kama wewe ni mtu unayelipenda Taifa hili, linda katiba na usikubali polisi washenzi wachezee katiba, na kudhalilisha muhimili wa mahakama.
 
Unamuelewesha huyo mpumbavu?
 
Kwa sasa neno haki limeanza kushika nguvu dhidi ya hadaa ya muda mrefu ya amani. Muda mrefu amani imetumika kama kitisho cha kudai haki. Ila kizazi hiki sasa kimejua kina wajibu wa kupigania haki, kwani amani automaticaly itakuja kukiwa na haki.

Wananchi wote tudai HAKI, tusiwaruhusu wadhulumaji wa haki kujificha kwenye unafiki wa kutaja ovyo ovyo neno Amani.
 
Huyu Tlaahtlaah na nduguye Mwashambwa nao wanasemaje?
 
Mithali 29:2
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.

Kwa kweli hekima ya Sulemani inaishi mpaka leo. Tunaona leo kwenye nchi yetu watu wanavyougua kutokana na waovu wadhulumaji wa haki kushika madaraka.
 
Huyu Tlaahtlaah na nduguye Mwashambwa nao wanasemaje?


Hatutarajii kusikia lolote la maana kutoka kwao, kwa maana dhamira zao zinawaza uovu wakati wote, wakati wazalendo wa kweli wa nchi wanataka haki atamalaki katika Taifa ili kila mtu atendewe haki bila ya kujali asili yake, jinsia yake, mahali atokako, dini yake au uanachama wake wa kiasiasa.
 
Atakaye kupinga hoja hizi m lock, umeeleweka
 
Ishi sana mkuu, una hoja zenye mashiko
 
Huu wimbo wa amani bila haki unakaribia kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…