TANZIA Yona Fares Maro (MwanaJF na Muasisi wa Wanabidii) Afariki Dunia

TANZIA Yona Fares Maro (MwanaJF na Muasisi wa Wanabidii) Afariki Dunia

Yan ukishindwa kuhandle kitu bora utoke kuliko kutoa uhai,
Uhai kakupa Mungu usifanye kujitoa duniani kisa mtu au maumivu
Ukitoka kimbilia kwa Mungu, yeye ni Baba, kama ni baba anaelewa unapo potia, ukiweza kulia liaaa had uchungu uishe,(hata kama ww ni mwanaume liaa toa machoz jifungie mahali mlilie Baba yako, tusijifanye wagumu hadi kwa aliyetufinyanga) ukiweza funga mwambie Mungu nimeumia siwezi kulibeba hili, utaona kidogo kidogo unapona

Binadamu tunakutana duniani hapa hapa na tunaachana hapahapa
Ndio maana kiapo kinasema mpaka kifo kitakapo tutenganisha

Ina maana huko mbinguni huendi naye huyo mtu.
Hakuna mtu mwenye mbingu ya kukupeleka
Kila mtu anapito lake, kila mtu ana mahali analia na Mungu lakin jamani hakuna mwenye maisha yaliyo nyooka ni Mungu tu anatuvusha kuvuka kwenda mahali pengine

Watu wanalia watu wana maumivu mno lakin tujipeleke kwa Mungu anasikia

Polen wafiwa wote
 
Ndoa ni mwiba mkuu,bila ya kumshirikisha Mungu unaweza kufanya uamuzi wowote ule,hata kama utashirikisha marafiki,ndugu,wanasaikolojia,wachungaji na vitu vyote ujuavyo,usipokuwa karibu na Mungu ni kazi bure..
Hata kama,wangapi tunaona wanaachana kwani hiyo yake ndo ya kwanza kuwa na changamoto kama zake?Hakuna utetezi wa maamuzi ya kujiua regardless unapitia yapi
 
Alikuwa guesthouse! Ambaye hayajamkuta anaweza kudhani jamaa alikuwa Mpuuzi la hasha akinamama wana viboko ambavyo vikikuingia unaweza fanya uamuzi kama huo
Ah ah ah ah nacheka kama mazuri, comment yako imenifanya nicheke.
 
Kumbe ule utafiti unaosema wanaume wengi hufa mapema kwa msongo wa mawazo ni kweli..kwa hili naona marehemu ameshindwa kuvumilia kuumia ameamua ajimalize pole yao familia
Wengi sana wanalia ndani yao, hawana mtu wa kumwambia, bora sis wamama tukilia tukilia tunapunguza vingi.

Mungu awasaidie waume zetu
 
Daahh mdau

Yaani ninyi viumbe siwaamin milele mwanzo wa ulimwengu tuu mlidanganyika
Hakika sintooa cha msingi ni watoto tuu ninyi kupiga tuu
 
Walio kwenye ndoa zinafukuta wanatamani kutoka, walio Nje wanatamani kuingia kwa kila namna. Duh!

Pole wafiwa, RIP marehemu.
Ndivyo inavyokuwa. Cha msingi umtambue mwenza wako mapema. Mwingine kbl ya kufunga ndoa amekuwa amekuonyesha ishara amekuonyesha huyu siyo mke lkn utakuta mtu anabeba hivyo hivyo akiamin atabadilika ndiyo matokeo yanakuwa hivi.
Wanawake ni wazuri kwa kula na kusepa na siyo kuweka ndani. Aise it is so sad
 
Ndo ushangae jamani.
Ugonjwa wa kupenda ni mbaya sana. Mimi kuna mwanamke mmoja kutokana na ugonjwa wa kupenda amechukua fedha zake akawekeza kwangu millions na mimi kusema kweli kila nikijitahidi nimpende nashindwa yan sometime namuomba Mungu anishushie upendo nimpende tu lakini daah namuachia Mungu.

Sasa huko kwenye mitandao naye kawa kama chizi hadi sometime namuita home kumtuliza ila sijui nitafanyeje kumpenda jamani jamani! Kuna muda natamani hata aniendee kwa mganga basi nimpende tu! Mwanamke ana elimu nzuri ya masters. Umbo zuri nilimkuta bado hajatumika ila upendo kweli nasema kutoka moyoni haupo haupo haupo. Ee Mungu nisamehe tu kwa dhambi hii ila sitaki nimuweke kwangu kisha nianze kufanya mambo ya ajabu maana simpendi na nimeshindwa hata kudanganya upendo.

Hata huyu jamaa aliyejiua naona mwanamke hakumpenda ila alilazimisha tu. Aisee usiombee uwe na moyo huo!
 
Wengi sana wanalia ndani yao, hawana mtu wa kumwambia, bora sis wamama tukilia tukilia tunapunguza vingi.

Mungu awasaidie waume zetu
Mnatutesa sana nyie wanawake. Inafika kipindi mpaka tunalia kwa ajili yenu. Mm mwenyew naandika lkn nina mzigo mzito sana kwenye moyo wangu. Usione wanawaume tupo barabaran lkn......... Mungu ndiye anajua
 
Back
Top Bottom