Kuna taarifa kuwa Yona Fares Maro ambaye ni mwanaJF na muasisi wa Wanabidii, Google Group amefariki dunia jana tarehe 12 January 2018 baada ya kunywa sumu.
View attachment 674668
Uamuzi wa kunywa sumu ulitokana na ugomvi baina yake na mke wake nyumbani kwao Mbeya.
Mazishi yatafanyika Jumatatu tarehe 15 Januari Kijijini kwao Mowo, Old Moshi - Kilimanjaro.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina Lake lihimidiwe.
Natoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu
Chanzo ni ukurasa wa Facebook wa dada yake na Yona:
Janet Fares Maro
Huu ndio ujumbe aliouacha marehemeu nyuma ya kifo chake
Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi.
Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi.
Sasa nipumzike nimwache mke wangu Eng Mloelya na mchepuko wake Eng Lossy wa Idara ya Maji Mbeya waendelee!