Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190930_125128.jpg
Timu 16 zilizofuzu Play off game ambazo mojawapo ndio itapangiwa Yanga*

1.RS Berkane (Morroco)

2.Al Masry(Egypt)

3.Hassania Agadir (Morroco)

4.Zanaco (Zambia)

5.Enugu Rangers (Nigeria)

6.Djoliba (Mali)

7.Esae(Benin)

8.DC Motema Pembe (DRC)

9.FC San Pedro(Ivory Coast)

10.Bandari (Kenya)

11.Bidvest Witts(South Africa)

12.Ts Galaxy (South Africa)

13.ploline (Uganda)

14.Triangle (Zimbabwe)

15.Pyramids (Egypt)

16.Paradou (Algeria)

Kulingana na taratibu za uchezeshaji draw za CAF Yanga inaweza kupangwa na yeyote kuanzia no 7 mpaka 16.

Yangafulldozz
 
20190930_131126.jpg

Mamelodi Sundowns klabu toka South Africa yaivunja rekodi yetu kwenye Klabu Bingwa barani Africa ambayo ilidumu miaka kumi.

Ushindi wa uwiano 16-1 iliyoupata klabu ya Mamelodi Sundwon dhidi ya klabu toka Sychells ijulikanayo Kama Coto d`or umevunja record iliyokua ikishikiliwa na Yanga kuifunga kwa uwiano goli 14-1Timu ya Etoile d`or toka Commoro msimu wa 2009 katika michuano ya klabu bingwa barani Africa,michuano inayoandaliwa na CAF.

Katika mechi ya awali Yanga ilishinda goli 8-1 Jijini Dar huku mshambuliaji wake raia wa Kenya Boniface Ambani akifunga magoli manne pekee katika mechi hiyo na katika mechi ya marudiano iliyofanyika nchini Commoro Yanga ilishinda kwa magoli 6-0 huku mshambuliaji wake Mrisho Ngasa akifunga magoli manne pekee pia na kufanya uwiano kua 14-1 ni record iliyodumu kwa zaidi ya miaka kumi mpaka Mamelodi Sundowns kuivunja hivi majuzi.

Congratulations to Mamelodi Sundowns..
Hii ndio Yanga.
 
TUNAHITAJI KUFUNGA MABAO MENGI NYUMBANI "ZAHERA
.
Baada ya Yanga kuondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa na kushushwa kombe la Shirikisho, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema ili kuwa na uhakika wa kutinga makundi watahitaji kufunga mabao mengi nyumbani

Zahera ambaye timu yake iliondolewa na Zesco kwa kufungwa mabao 2-1, amekiri kuwa uhaba wa mabao nyumbani umewasababishia kushindwa kuingia makundi ligi ya mabingwa "Hakufunga mabao mengi, tulikuwa na changamoto za hapa na pale kwenye safu yetu ya ushambuliaji lakini sasa nadhani tumeanza kuwa vizuri," amesema "Hatupaswi kurudia makosa tuliyofanya ligi ya mabingwa, tunahitaji kufunga mabao zaidi ya mawili nyumbani ili kupunguza presha ya mchezo wa ugenini"

Yanga inasubiri kumjua mpinzani wake droo ikitarajiwa kufanywa wiki ijayo nchini Misri

Jambo la uhakika ni kuwa Yanga itaanzia nyumbani na baadae kwenda kumalizia ugenini

Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa beki wake kisiki Lamine Moro aliyepewa kadi mbili za njano kwenye mchezo dhidi ya Zesco.

Source. Yangafulldoz.
 
Asante kwa ma News motomoto na ya uhakika ya chama letu kubwa la wananchi. Nnachofurahi ni kuona sasa timu imeanza kuwa tamu
 
20191001_085600.jpg
Baada ya Maboresho ya Ratiba ya Ligi kuu Tanzania Bara sasa rasmi Mechi zetu mbili zijazo

Alhamis : 03.10.2019
Saa 10 jioni
Yanga v/s Polisi Tz

Uwanja wa Uhuru

Jumapili : 06.10.2019
Saa kumi jioni
Yanga v/s Coastal

Uwanja wa Uhuru

Yangasc.
 
20191001_090221.jpg

MAKAME AWAOMBA RADHI MASHABIKI YANGA
.
Kiungo wa Yanga, Abdulaziz Makame ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo, baada ya juzi kujifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Mchezaji huyo alisema tukio hilo ni baya zaidi kutokea kwake tangu alipoanza kucheza soka.

Akizungumza Makame amewataka mashabiki kusahau bao hilo na kujiandaa vyema kwa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Makame aliyecheza kwa kiwango bora katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini, alijifunga bao dakika ya 78 katika harakati ya kuokoa kiki ya mpira wa krosi iliyopigwa upande wa kushoto na winga Quadri Aladeokun.

Akizungumzia bao hilo, Makame alisema lengo lake lilikuwa kutoa mpira nje baada ya kuona anakabiliwa na wachezaji wawili wa Zesco nyuma yake. "Nilikwenda kasi kuzuia mpira baada ya kuona nyuma yangu kuna wachezaji wa Zesco, nikiwa na uhakika wa kutoa nje bahati mbaya nikajifunga,"alisema Makame.

Kiungo huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Mafunzo ya Zanzibar, alisema kilichotokea ni sehemu ya mchezo na amewataka wadau wa klabu hiyo kujipanga kwa Kombe la Shirikisho.

Makame alisema Yanga inapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kwa kuwa mashindano hayo yanashirikisha timu zenye uzoefu, hivyo wanapaswa kujiandaa kikamilifu.

Kiungo huyo alikuwa nyota wa mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam waliotoka sare ya bao 1-1.

Baada ya mchezo huo, Kocha wa Zesco, George Lwandamina alisema Makame ni mchezaji wa aina yake na alikuwa kikwazo kwa timu yake kupata ushindi.

Lwandamina alisema tukio la kujifunga linaweza kumpata mchezaji yeyote na sehemu ya mpira. "Ni tukio la bahati mbaya yule kijana ni hodari sana katika nafasi ya kiungo" "Jambo hili lingeweza pia kumpata mchezaji wangu. Lakini wenye nafasi ya kumjenga au kumbomoa ni wachezaji wenzake na benchi la ufundi la Yanga kwa namna watakavyopokea tukio lile," alisema Lwandamina.

Mwanaspoti
 
TUNAHITAJI KUFUNGA MABAO MENGI NYUMBANI "ZAHERA
.
Baada ya Yanga kuondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa na kushushwa kombe la Shirikisho, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema ili kuwa na uhakika wa kutinga makundi watahitaji kufunga mabao mengi nyumbani

1569911447867.png
 
Back
Top Bottom