MJUE MWINYI ZAHERA
Anaitwa Mwinyi Zahera alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962. Ilipofika mwaka 1975 Zahera alianza kucheza mpira akiwa na miaka 13 katika klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka1980.
Baada ya hapo akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu,
Akajiunga na chuo cha Teknolojia(ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Mr. Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka la kulipwa. .
Alifika Ulaya na kusajiliwa na Antwerp Fc ya Ubelgiji alicheza kwa miaka miwili kabla ya kumaliza mkataba wake kumalizika na kwenda Ufaransa alikocheza katika timu za daraja la pili Amiens Fc, Beauvais Fc kisha Abbeville hadi alipostaafu soka.
Baada ya hapo Zahera alianza mafunzo ya Ukocha ambako alitunukiwa Diploma na Leseni A ya Shirikisho la soka Ulaya(UEFA) baadae akaenda kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kwa mafanikio makubwa kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2010 kisha akatimkia Ubelgiji kwenda kuifundisha AFC Tubize kwa msimu mmoja na baadaye kurudi tena Ufaransa akiifundisha klabu ya Douai Fc kwa misimu miwili kabla hajarejea tena AFC Tubize kama kaimu kocha mkuu wa klabu hiyo ilipofika mwaka 2014 alirejea nchini kwao Congo DR na kuifundisha klabu ya DC Motema Pembe mpaka mwaka 2016.
Tar. 30 September/2017 Zahera alitangazwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Congo DR akiwa chini ya kocha mkuu Frolent Ibenge Na ilipofika 25April 2018 Zahera alijiunga rasmi Dar es Salaam Young Africans Sports Clubs "Yanga Sc" kama kocha mkuu akirithi mikoba ya kocha George Lwandamina(Chicken) .
Huyu ndio Papaa Mwinyi Zahera Mcongoman mwenye uraia wa Ufaransa kwa sasa ana miaka 56, Usisahau Oktoba19 ni birthday yake. Natumai sasa walau umemjua vema kocha wetu.
yangaafuldozz