Uongozi wa
@yangasc umekiri kuwa usajili uliofanywa dirisha lililopita haukumaliza changamoto katika baadhi ya nafasi
Na moja ya sababu inayotajwa ni uamuzi wa kumuachia Mwalimu Zahera kusimamia zoezi lote la usajili peke yake
Yanga ina nafasi nyingine ya kuboresha kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa hivi karibuni
Wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka wametoa maoni juu ya aina ya maboresho ambayo wanadhani yataisaidia Yanga
Miongoni mwa wadau hao ni Ally Mayay ambaye ni mchambuzi wa soka lakini pia akiwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Yanga
Mayay aliyewahi kutamba akiwa kiungo mkabaji Yanga, anaamini yanahitajika kwa kuongeza washambuliaji wa pembeni (mawinga) na mshambuliaji wa kati
.
..."Ni kweli kabisa, kwa uhalisia mpaka sasa katika mechi ambazo Yanga imecheza hakuna mshambuliaji ambaye ana uhakika kama atapata mipira miwili au mitatu anafunga mabao. Hili ni eneo ambalo Inahitaji kutulia,"
.
alisema Mayay "Tangu Tambwe aondoke ambaye anajua kazi yake ni kufunga tu au Makambo bado haIjapata mtu sahihi, Sadney sio mshambuliaji wa ubora huo wala Balinya (Juma) yule ni mshambuliaji wa nyuma ya mshambulaiji wa mwisho au ashambulie kutokea kushoto kama alivyokuwa anatumika katika klabu yake ya nyuma.
.
..................."Lakini pia Yanga haina winga mwenye makali, hii ni asili ya Yanga kuwa na mawinga wakali tangu enzi za kina Lunyamila (Edibily) hadi alipotokea Msuva (Simon), baada ya hapo haina mtu wa ubora huo itafute winga wa kulia. 'Pia itafute winga wa kushoto sioni kama Sibomana ni winga halisi labda iwe inamtumia kulingana na mfumo ili aweze kushambulia akitokea kati, lakini ninavyoona itafute mtu kama Singano (Ramadhan) au Kichuya (Shiza)
Yangafulldoz