Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191109_054726.jpg
 
MWAKALEBELA AFUNGA MJADALA WA MWINYI ZAHERA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuungana ili kuhakikisha timu inafanya vyema na wasikubali kuyumbishwa na yanaoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusu kocha Mwinyi Zahera

Zahera ambaye hivi karibuni mkataba wake ulisitishwa na uongozi wa Yanga, umekuwa akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari akitoa tuhuma nzito kwa uongozi wa Yanga

Mwakalebela amesema Wanayanga hawapaswi kukubali kuyumbishwa, maamuzi yameshafanyika na kinachotakiwa waangalie mbele

Aidha amesisitiza kuwa Yanga haina muda wa kujibu tuhuma zake "Hatuna sababu ya kujiingiza kwenye mijadala ambayo ina lengo la kutugawa. Kwa sasa akili yetu ipo kwenye mechi dhidi ya Ndanda na hatuna muda wa kumjadili mtu ambaye hayupo kikosini. "Zahera hawezi kututoa kwenye reli, tunapambana kusaka ushindi kwenye mechi yetu Mtwara. Alikuwapo kikosini, kama kulikuwa na matatizo kwanini hakuzungumza hadi asubiri alipotimuliwa? Hatupo tayari kumjibu ili asitupotezee dira na mipango yetu," amesema.
Hili jukwaa naona wewe tu ndo unaranda randa hapa!!! Mtani kwani ukiachana na yanga utakufa? [emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
MKWASA APONGEZA WACHEZAJI YANGA.
Pamoja na kuwa na kikosi kwa muda mfupi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewapongeza wachezaji kwa kutimiza maagizo aliyowapa mazoezini na hatimaye kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc

Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara, Mkwasa alisema falsafa yake ni soka la kushambulia na hicho ndicho walichokifanya jana "Ingawa tumekuwa pamoja kwa muda mfupi, vijana wamefanya vizuri, tunahitaji kucheza kwa kushambua zaidi" "Tumecheza vile tulivyokubaliana. Tulitengeneza nafasi kadhaa lakini muhimu zaidi ni kuwa tumeshinda" "Ndanda hawakuwa wabaya, sifahamu kwa nini hawapati matokeo mazuri kwenye mechi zao, lakini ni timu nzuri," alisema

Kugawa majukumu mipira ya adhabu

Mkwasa amesema tukio la wachezaji wake kugombea kupiga mipira ya adhabu ameliona, atalifanyia kazi "Nimekuwa na wachezaji mazoezini kwa siku moja tu, changamoto zote zinazoonekana tutazifanyia kazi" "Tutagawa majukumu kwa kila mchezaji ili kuepusha malumbano ya hapa na pale"

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo lilifungwa na Patrick Sibomana kwa mpira wa adhabu ambao awali ulipigwa na David Molinga lakini mwamuzi akaamuru upigwe tena baada ya wachezaji wa Ndanda kuwahi kutoka kwenye ukuta kabla ya mpira kupigwa

Kabla ya Sibomana kupiga mpira huo kulikuwa na mvutano kati ya Molinga na wachezaji wengine ambao hawakutaka apige yeye na badala yake amwachie Sibomana uamuzi ambao uliinufaisha Yanga.
 
MWAKALEBELA AFUNGA MJADALA WA MWINYI ZAHERA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuungana ili kuhakikisha timu inafanya vyema na wasikubali kuyumbishwa na yanaoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusu kocha Mwinyi Zahera

Zahera ambaye hivi karibuni mkataba wake ulisitishwa na uongozi wa Yanga, umekuwa akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari akitoa tuhuma nzito kwa uongozi wa Yanga

Mwakalebela amesema Wanayanga hawapaswi kukubali kuyumbishwa, maamuzi yameshafanyika na kinachotakiwa waangalie mbele

Aidha amesisitiza kuwa Yanga haina muda wa kujibu tuhuma zake "Hatuna sababu ya kujiingiza kwenye mijadala ambayo ina lengo la kutugawa. Kwa sasa akili yetu ipo kwenye mechi dhidi ya Ndanda na hatuna muda wa kumjadili mtu ambaye hayupo kikosini. "Zahera hawezi kututoa kwenye reli, tunapambana kusaka ushindi kwenye mechi yetu Mtwara. Alikuwapo kikosini, kama kulikuwa na matatizo kwanini hakuzungumza hadi asubiri alipotimuliwa? Hatupo tayari kumjibu ili asitupotezee dira na mipango yetu," amesema.
Safi
 
20191112_053747.jpg
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema atahakikisha timu hiyo inarejea kucheza staili ya kushambulia muda wote ili kuvuna mabao mengi.

Mkwasa juzi aliiongoza Yanga kuvuna ushindi wa bao 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Nagwanda Sijaona, Mtwara.

Kocha huyo wa mpito alichukua nafasi ya Mkongomani, Mwinyi Zahera aliyetimuliwa katikati ya wiki iliyopita.

Ushindi huo uliifanya Yanga kufikisha pointi 10, baada ya kucheza michezo mitano, ikishinda mitatu, sare mmoja na kupoteza idadi kama hiyo.

Mkwasa ameahidi kurudisha falsafa ya kucheza kwa kushambulia dakika zote

Alisema kikosi hicho kimejipanga kuhakikisha kinashinda michezo yake yote ya kiporo ili kujikusanyia pointi zitakazoweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo. "Nashukuru vijana wangu kwa kufuata maelekezo yangu na kufanikisha ushindi katika mchezo huo,japo nilikuwa na muda mchache na timu,lakini vijana walinipa ushirikiano na kufanya tulichopanga. "Lengo ni kurudisha falsafa yetu ya kucheza kwa kushambulia, wapenzi wetu wamezoea kuiona Yanga ikimnyima raha mpinzani, tutahakikisha tunafanya hivyo ili kurudisha hadhi yetu na kupata mabao mengi zaidi," alisema.

Mkwasa alisema anataka kukifanya kikosi hicho kuwa tishio kwa wapinzani na kurudi katika mbio za kufukuzia taji la Ligi Kuu Bara walilipoteza misimu miwili iliyopita.
 
20191114_060428.jpg

Kikosi Cha Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara @yangasc Kinatarajia Kuanza mazoezi leo ikiwa ni Siku moja baada ya kikosi hicho kurejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mtwara. .

Kikosi Cha Wababe hao kinajifua kuelekea mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara Dhidi Ya maafande wa JKT Tanzania, Mchezo unaotarajiwa kufanyika November 23, 2019 Kwenye Uwanja Wa Uhuru. .

Aidha Afisa Habari wa Klabu Ya Yanga @hbumbuli Amebainisha kuwa, Uongozi wa Klabu hiyo Upo katika mchakato wa Kuandaa Mchezo mmoja wa Kirafiki kabla ya kuwavaa JKT Tanzania.
 
20191114_060759.jpg
Uongozi wa @yangasc umekiri kuwa usajili uliofanywa dirisha lililopita haukumaliza changamoto katika baadhi ya nafasi

Na moja ya sababu inayotajwa ni uamuzi wa kumuachia Mwalimu Zahera kusimamia zoezi lote la usajili peke yake

Yanga ina nafasi nyingine ya kuboresha kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa hivi karibuni

Wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka wametoa maoni juu ya aina ya maboresho ambayo wanadhani yataisaidia Yanga

Miongoni mwa wadau hao ni Ally Mayay ambaye ni mchambuzi wa soka lakini pia akiwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Yanga

Mayay aliyewahi kutamba akiwa kiungo mkabaji Yanga, anaamini yanahitajika kwa kuongeza washambuliaji wa pembeni (mawinga) na mshambuliaji wa kati
.
..."Ni kweli kabisa, kwa uhalisia mpaka sasa katika mechi ambazo Yanga imecheza hakuna mshambuliaji ambaye ana uhakika kama atapata mipira miwili au mitatu anafunga mabao. Hili ni eneo ambalo Inahitaji kutulia,"
.
alisema Mayay "Tangu Tambwe aondoke ambaye anajua kazi yake ni kufunga tu au Makambo bado haIjapata mtu sahihi, Sadney sio mshambuliaji wa ubora huo wala Balinya (Juma) yule ni mshambuliaji wa nyuma ya mshambulaiji wa mwisho au ashambulie kutokea kushoto kama alivyokuwa anatumika katika klabu yake ya nyuma.
.
..................."Lakini pia Yanga haina winga mwenye makali, hii ni asili ya Yanga kuwa na mawinga wakali tangu enzi za kina Lunyamila (Edibily) hadi alipotokea Msuva (Simon), baada ya hapo haina mtu wa ubora huo itafute winga wa kulia. 'Pia itafute winga wa kushoto sioni kama Sibomana ni winga halisi labda iwe inamtumia kulingana na mfumo ili aweze kushambulia akitokea kati, lakini ninavyoona itafute mtu kama Singano (Ramadhan) au Kichuya (Shiza)

Yangafulldoz
 
Back
Top Bottom