Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NINJA ASHANGAA MECHI YA YANGA DHIDI YA KMC
Beki wa LA Galaxy ya Marekani, Abdallah Shaibu 'Ninja' juzi alikuwepo jukwaani akishuhudia Yanga ikilazimishwa sare 1-1 na KMC
Ameeleza kushangazwa jinsi timu yake hiyo ya zamani ilivyocheza soka la kupooza.
Ninja aliyeichezea Yanga kabla ya kujiunga na LA Galaxy mwanzoni mwa msimu amerejea nchini katika mapumziko wakati huu Ligi ya Marekani imesimama kupisha majira ya baridi.
Akizungumzia mechi hiyo, Ninja alisema katika mchezo huo ameona walikuwa wanacheza kwa kupooza kama vile wachezaji wamechoka, kitu ambacho si kizuri kwa Yanga inayohitaji ubingwa. "Si Yanga wala KMC, walicheza kwa kupooza sana, imeonekana kama wachezaji wamechoka pengine ratiba ya ligi inawabana, ila wanahitaji kujitofautisha na timu nyingine ili kuchukua ubingwa," "Wachezaji wazawa wajaribu kuwapa nafasi, kwani wanakuwa wanajua ligi ilivyo kuliko wageni ambao nimeona wanakwama kidogo," alisema Ninja.
Jambo lingine ambalo alikuwa makini sana kulifafanua kwamba hataki kuingilia majukumu ya benchi la ufundi ila alishauri wachezaji wangecheza kwenye namba zao akimtolea mfano Jafary Mohamed
Mwanaspoti
Uwiii!! Mi sipo Mkuu kwenye hayo magroup.Naomba uniunge kwny group la yanga...0717550291
Mchukuweni na Ally Kiba basi Shadeeya ni winga hatari sana tena ni shabiki lialia wa Chura FCWINGA WA COASTAL AJIPELEKA YANGA
KUELEKEA usajili wa dirisha dogo, winga wa timu ya Coastal Union, James Kihimba, ametamba kuwa na namba katika kikosi cha Yanga baada ya kuanza kunyemelewa na viongozi wa klabu hiyo.
Kihimba ambaye msimu uliopita alichezea Biashara United, mkataba wake na Coastal Union unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Akizungumza na BINGWA jana, mchezaji huyo alisema, kuna mazungumzo yanaendelea kati yake na Yanga, endapo mambo yatakwenda vizuri hatasita kujiunga na timu hiyo kwa sababu ni moja ya ndoto zake.
Alisema aliwahi kuzungumza na Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, siku walipocheza na Wanajangwani hao katika mechi ya kirafiki hivi karibuni. “Siku ile tuliyocheza na Yanga pale Taifa, mechi ilivyoisha yule mwenyekiti wao (Dk. Msolla), alinifuata na kuniambia nimefanya kazi nzuri, tena kama kutakuwa na uwezekano dirisha dogo watanichukua,” alisema. “Yanga kuna wachezaji wengi lakini nafasi yakucheza naona ipo kwa sababu najua ninachokitafuta, nitakomaa hadi nipate namba kikosi cha kwanza, muhimu ni kujituma tu na maelekezo ya mwaliamu,” alisema.
Alieleza kuwa hakuna kitakachomzuia kutoka Coasta Union kwa sababu mkataba wake una kipengere cha kumruhusu kuondoka muda wowote. “Nina mkataba wa mwaka mmoja, unamalizika msimu huu lakini una kipengele kinachoniruhusu kuondoka, nimefanya hivyo kwa sababu mara kwa mara naenda kufanya majaribio nje ya nchi,” alisema.
@Yangafulldozz
Usogee karibu na hospital kabisaYap yap!!! Naisubiria hiyo siku Mtani.
Patachimbika. í ½í²í ½í²í ½í²
😀😀 Usijali Mtani.Usogee karibu na hospital kabisa
Lengo la TFF ni kupiga pesa tuTPLB YASISITIZA MECHI YA WATANI WA JADI ITAPIGWA JANUARY 4
Pamoja na uwepo wa michuano ya kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka, Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesisitiza haitafanya mabadiliko ya tarehe ya mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga
Mchezo huo umepangwa kupigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto amesema wamepeleka mapendekezo kwa waandaaji wa michuano ya kombe la Mapinduzi ili ichezwe kwa mfumo wa mtoano
Hata hivyo amesema vilabu vya Simba na Yanga vitalazimika kurejea nchini kucheza mchezo baina yao January 04 "Tulichofanya sisi ni kuwasiliana na viongozi wa kamati ya maalum inayosimamia michuano ya Mapinduzi, ili watupe maoni yao kuhusu tariba ya ligi hapa Tanzania Bara," amesema Mguto "Tumeomba michuano ya Mapinduzi iwe ya mtoano ili timu za huku ziweze kucheza mechi zake mara zitakapotoka, lakini kwa Simba na Yanga hata kama zitaingia hatua ya nusu fainali au robo zitatakiwa zirudi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, hivyo hatutabadilisha"
Hakika Mkuu.Lengo la TFF ni kupiga pesa tu