Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

LEO HIYO 🤔🤔🤔🤔

👇👇👇

MSOLA: TUMERITHI MADENI MAKUBWA, HAKUNA HELA INAYOLIWA


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msola ametoa ufafanuzi juu ya mapato ya matumizi tangu walipoingia madarakani mwezi Juni mwaka huu huku akisema hakuna pesa inayoliwa.

Msola amesema gharama za kuendesha timu ni kubwa kuliko mapato yanayoingia huku wakiwa wamerithi madeni makubwa kutoka katika uongozi uliopita.

Mwenyekiti huyo ametaja madeni makubwa ya aina nne waliyo warithi ambayo ni kama ifuatavyo-
1.Serikali (Mamlaka ya Mapato Tanzania 'TRA' shilingi milioni 800)
2.Ada ya uhamisho ya wachezaji shilingi waliosajiliwa miaka miwili ilyopita shilingi milioni 254.
3. Madeni ya makocha na wachezaji waliopita (Hans Van Pluijm, George Lwandamina, Youthe Rostand, Donald Ngoma na Obrey Chirwa) jumla shilingi milioni 600.
4. Watu binafsi shilingi milioni 237
5. Gharama za Usajili wa timu za wakubwa na ile ya Wanawake shilingi milioni 600.

Msola ametaja vyanzo vya mapato vya klabu hiyo ambayo ni SportPesa, KCB, Vodacom, Azam TV, GSM, Yanga TV na kampuni ya Maji ya Afya ambayo kwa mwaka wanapata shilingi bilioni mbili wakati gharama za kuiendesha timu ni bilioni nne. "Nimeamua kuja kwenu Waandishi ili nitoe ufafanuzi juu ya mapato na matumizi ya klabu yetu. Tulivyoingia madarakani tulikuta timu madeni makubwa ambayo tumejitahidi kuyapunguza huku bado tukitakiwa kuiendesha timu," alisema Msola.

@Yangadaima
 
20191210_162049.jpg
HATUNA MPANGO WA KUMUACHA LAMINE - YANGA
Uongozi wa klabu Yanga umesema hauna mpango wa kumuacha beki wao kisiki Lamine Moro ambaye aliandika barua ya kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya mishahara

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amekiri beki huyo kuwa na madai ya mishahara miwili na sio mitatu "Lamine bado ni mchezaji wetu kwani ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Madai yake ya mishahara ya miezi miwili pamoja na wachezaji wengine wote watalipwa leo," amesema

Ataja sababu ya kumtema Sadney

Aidha Dk Msolla amesema uongozi umeamua kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake Sadney Urikhob kutokana na uwezo wake kutoendana na matarajio ya klabu

Dk Msolla amesema Sadney aliomba mkataba wake kuvunjwa na uongozi uliridhia kwa kuwa hakuweza kufikia matarajio ya timu "Tumemwachia Sadney kwakuwa uwezo wake ni mdogo lakini tunapambana kumzuia Lamine Moro asiondoke. Mpira ni mchezo wa wazi , uwezo wa beki huyu kila mtu ameuona"

@Yangadaima
 
YANGA KUCHEZA MECHI NNE KABLA YA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA SC

Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa January 04 kwenye uwanja wa Taifa

Kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, Yanga inatarajiwa kucheza mechi nne kabla ya kukabiliana na watani zao wa jadi

Wataanza na mchezo wa raundi ya tatu kombe la FA utakaopigwa kati ya Disemba 21/22 kwenye uwanja wa Uhuru

Baadae Yanga itaelekea mkoani Mbeya ambako Disemba 24 itaumana na Mbeya City uwanja wa Sokoine

Simu tatu baadae, Disemba 27 itarudi uwanja wa Sokoine kuikabili Tanzania Prisons

Baada ya michezo hiyo Yanga itarejea jijini Dar ambapo Disemba 30 itacheza na Biashara United
 
MOLINGA HAKUOMBA KUVUNJA MKATABA NA YANGA

Mshambuliaji David Molinga sio miongoni mwa walioandika barua ya kuvunja mikataba yao na Yanga kama ilvyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema mchezaji huyo aliomba ruhusa kwenda Ufaransa kumuuguza mwanawe

Molinga juzi alifika Makao Makuu ya klabu kuomba ruhusu na wakati huo akifuatilia VISA

Dk Msolla amesema kama VISA haitapatikana kwa haraka Molinga ameahidi kuendelea na mazoezi na wachezaji wengine ambao wamerejea kujifua jana baada ya mapumziko ya siku tano

Yanga imethibitisha ni Sadney Urikhob na Lamine Moro pekee ambao waliandika barua ya kuvunja mikataba yao

Sadney ameruhusuwa kuondoka baada ya uongozi kutokuwa na mpango nae lakini Lamine bado anahitajika ambapo Dk Msolla amesema watamshawishi mchezaji huyo aendelee kubaki huku akiahidi kulipa madai yake yote leo sambamba na wachezaji wengine.
 
MCHAKATO WA MABILIKO YA UENDESHAJI WA CLUB YANGA KUKAMILIKA MAY 2020

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hadi kufikia mwezi May 2020 Yanga itakuwa imebadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka wa sasa (mfumo wa wanachama) kuwa mfumo wa hisa

Dk Msolla aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili timu hiyo "Nawapa ahadi wanachama, ifikapo mwezi Mei 2020 tutabadili mfumo wa klabu kuwa wa uwekezaji. Tukishirikiana vyema na wanachama tutalifanikisha hili katika muda huo"

Mapema Dk Msolla alibainisha changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga huku akitaja timu hiyo kuwa na madeni yanayozidi Tsh Bilioni mbili huku mapato yakiwa hayatoshi

Yanga inakabiliwa na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya wachezaji na makocha hadi miaka mitatu nyuma

Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio hitaji la wengi wanaoamini Yanga itaweza kusimama.
 
MCHAKATO WA MABILIKO YA UENDESHAJI WA CLUB YANGA KUKAMILIKA MAY 2020

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hadi kufikia mwezi May 2020 Yanga itakuwa imebadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka wa sasa (mfumo wa wanachama) kuwa mfumo wa hisa

Dk Msolla aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili timu hiyo "Nawapa ahadi wanachama, ifikapo mwezi Mei 2020 tutabadili mfumo wa klabu kuwa wa uwekezaji. Tukishirikiana vyema na wanachama tutalifanikisha hili katika muda huo"

Mapema Dk Msolla alibainisha changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga huku akitaja timu hiyo kuwa na madeni yanayozidi Tsh Bilioni mbili huku mapato yakiwa hayatoshi

Yanga inakabiliwa na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya wachezaji na makocha hadi miaka mitatu nyuma

Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio hitaji la wengi wanaoamini Yanga itaweza kusimama.
Tuupe sapoti uongozi wetu,unahangaika sana na unapitia ktk kipindi kigumu sana,tutapita tu
 
20191213_062757.jpg
Klabu ya Yanga imemsajili Tariq Seif Kiakala kutoka klabu ya Dekernes Fc ya nchini Misri

Tariq aliwahi kuzitumikia Stand United na Biashara United kabla ya kutimikia Misri ambako alijiunga na timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili

Tariq ameonyesha kiwango kizuri huko Misri
Katika maandalizi ya msimu mpya, Tariq alicheza michezo 7, alifunga magoli 5 na kutoa pasi 3 za magoli

@Yangasc.
 
Back
Top Bottom