Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

AUSSEMS AMEOMBA KAZI YANGA SC

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Patrick Aussems ni miongoni mwa makocha walioomba nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga

Tetesi zinazomuhusisha kutua Yanga zilianza kushika kasi juzi, hatimaye jana uongozi wa Yanga umetoa ufafanuzi kuhusu ukweli wa suala hilo.

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Aussems ametuma CV zake akiomba nafasi hiyo inayokaimiwa na kocha Charles Mkwasa "Kocha Aussems ni miongoni mwa waliotuma maombi kuwania nafasi ya kuwa kocha Mkuu wa Yanga. Hivyo ni jukumu la Kamati ya Ufundi kuamua, kama wataona anafaa basi tutaingia nae kandarasi," amesema

Katika hatua nyingine, Bumbuli amesema usajili unaofanywa na Yanga sio kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa January 04 2020.

Amesema usajili huo unalenga kuboresha nafasi ambazo zilionekana kuwa na mapungufu.

Bumbuli ameongeza kuwa wachezaji wote wanaosajiliwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi.

Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa nyota wanne, Haruna Niyonzima, Tariq Seif, Ditram Nchimbi na Adeyum Saleh.

@Yangadaima
 
Kweli Mkuu ni jambo la kujiuliza. Na ni swali la msingi ambalo hadi sasa nadhani halijapatiwa jibu au majibu husika
Hapa napata shaka isije mwisho wa siku akasema hilo la usajili ndio lilikuwa jukumu lake pekee mengine ni ya Klabu.
 
Huyu kocha Patrick mnamuonaje uwezo wake endapo tutampata wakuu!! Mi kama nina imani haba hivi
Mi naona sio mbaya labda shida ni ile waliyosema mikia (sina hakika huenda walimsingizia pia) kwamba ameshindwa kusimamia discipline ndani ya timu. Mana akishashindwa kuisimamia basi hakutakuwa na timu tena kwani kila mchezaji ataamua afanye kile akitakacho akitegemea amepata kocha poa.

Kama vp wampe nafasi tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…