POLISI TANZANIA, AZAM FC WAMALIZA SAKATA LA NCHIMBI
Baada ya wadau wa soka kupaza sauti kufuatia uamuzi wa TFF kumnyima leseni mshambuliaji Ditam Nchimbi kuitumikia Yanga kufuatia kuwekewa pingamizi na Polisi Tanzania, viongozi wa klabu ya Azam Fc na wale wa Polisi Tanzania pamoja na TFF wamekutana leo kumaliza sakata la mchezaji huyo
Habari njema ni kuwa mwafaka umefikiwa baada ya pande zote kukubaliana hivyo TFF itatoa leseni ya Nchimbi
Polisi Tanzania imeridhia Nchimbi aitumikie Yanga
Hivyo atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Simba kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumamosi, Januari 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa.
@Yangadaima