JANUARY 4 TUNAKUJA KIVINGINE 'MKWASA'
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kitakuwa sawa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Januari 04 uwanja wa Taifa.
Mkwasa amesema mpaka kufikia Jumamosi, wachezaji wake watakuwa wamepata muda wa kutosha kuweka sawa miili baada ya uchovu wa kucheza mfululizo "Kwa wanaodhani mchezo dhidi ya Simba tutacheza kama tulivyocheza na Biashara United wanajidanganya. Tuna siku tatu za kujiandaa na mchezo huo, tunahitaji kushinda hivyo tutapambana" "Wanachohitaji wachezaji wangu ni mapumziko ili kupoza miili yao. Tutakuwa tukifanya mazoezi lakini zaidi yatakuwa ya kufanya miili ya wachezaji irudi kwenye hali yake," amesema Mkwasa "Ninachowaambia mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi, timu itakuwa tofauti kabisa Januari 04".
Tariq, Nchimbi, Yikpe waongeza nguvu.
Jana TFF imeachia leseni ya Ditram nchimbi hivyo atakuwa na ruksa ya kucheza mchezo wa Jumamosi.
Lakini pia ITC ya mshambuliaji Yikpe Gnamien inatarajiwa kuwasili wakati wowote na hivyo nae atakuwa na nafasi ya kucheza mchezo huo.
Kuongezeka kwa washambuliaji hao kutabadili kabisa sura ya safu ya ushambuliaji ya Yanga.
@Yangafulldozz