Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Tuwe positive timu yetu naona inazidi kucheza mpira mzuri. Matokeo yatakuja tu na natumai tutaanza na singida, Azam kutufunga siyo ishu sana,ni timu inayoweza kumfunga yeyote. Cha msingi kingine timu yetu ikomae sana na FA hadi tubebe ubingwa ili tujiwekee nafasi ya kucheza kimataifa mapema.
 
Mbumbumbu mmemsikia huyo mwana dada kashauri washabiki wa timu zote za Afrika muige mfano wa sisi mashabiki wa Yanga!?.Hapo mwisho pia kawaambia BE NICE, BE LIKE YANGA. Ama kweli najivunia kuishabikia Yanga.
 

Attachments

  • VID-20200119-WA0050.mp4
    5.7 MB
TUTAREJEA TUKIWA IMARA 'SHIKALO'

Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amesema pamoja na kikosi chao kutokuwa na mwenendo mzuri, watarejea kwenye ubora wao tena wakiwa imara.

Yanga imecheza mechi tatu mfululizo za ligi kuu bila ya kupata ushindi, ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Simba kabla ya kupoteza michezo dhidi ya Kagera Sugar na Azam Fc.

Mlinda lango huyo wa Kimataifa wa Kenya amesema wakati mwingine ni lazima kupitia nyakati ngumu ili kutengeneza njia ya mafanikio "Tumeshushwa chini na tunapita kwenye wakati mgumu, lakini amini kila changamoto inakuwa na njia ya mafanikio, tutarejea tukiwa imara," ameandika Shikhalo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Leo Yanga itashuka kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida kuwakabili wenyeji wao Singida United katika mchezo ambao mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji ushindi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…