Imejengeka dhana kuwa Simba ndiyo ina-enjoy the highest proportion of fans hapa nchini kuliko Yanga.
Wengi tunalazimika kuamini kuwa dhana hii ni misleading kwa sababu kuu 2:
1. historia inaonyesha kuwa asili ya Yanga ni Watanzania asilia (natives) ambao proportionally ni wengi kuliko jamii zote nchini
2. wafuasi wa Yanga (labda kutokana na historia ya aina ya wafuasi wake) hawana makeke sana....hata pale timu inapokuwa na mafanikio
Sababu # 2 hapo juu inahanikizwa na tukio la hivi karibuni huko bungeni ambapo mbunge mmoja mnazi wa Yanga, ambaye hakutaka hata jina lake lijulikane publicly pamoja na Yanga kubeba kombe la Kagame, alitoa mwaliko kwa wabunge wenziwe wanazi wa Simba. Soma newspaper article hii hapa chini....
Simba wangekuwa wameshinda, hawa wanazi wote waliomo kwenye mwaliko uliotajwa hapa chini ungewasikia makeke yao!!!
Makeke haya ndiyo haswa yanayotafsiriwa (dhahiri kwa kupotoka) kuwa eti Simba ina wafuasi wengi kuliko watani wao Yanga.
Over to you Simba and Yanga fans........huu ndio mtizamo wangu mimi. Wewe je??
QUOTE
............Spika Makinda alisema kwa namna ya pekee Bunge linaipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa kwa mara ya nne baada ya kuifunga timu ya Simba juzi kwa taabu kwa goli 1-0 katika dakika ya 108 kwenye hiyo iliyochezwa kwa dakika 120 .
Spika Makinda alisema amepokea ujumbe mfupi kutoka kwa mbunge (hakumtaja) ukiwaalika wabunge kadhaa kwenye hafla maalum ya kusherehekea ubingwa wa Kagame.
Aliwataja wabunge hao wanaosemekana kuwa ni mashabiki wa Simba, kuwa ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Rage, Waziri wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), Samuel Sitta, Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM) Juma Nkamia, Mbunge wa Ilala (CCM) Musa Zungu, Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa (CCM) Job Ndugai, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Kapuya.
Wengine ni Mbunge wa Kinondoni (CCM) Iddi Azzan, Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema (CCM) William Ngeleja na Mbunge wa Gando (CUF) Khalifa Suleiman Khalifa, ambao alisema wamealikwa katika hafla ambayo haikulezwa itafanyika sehemu gani.UNQUOTE