Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

"Kikubwa nnachoweza kusema nawaomba wana Yanga tuwe watulivu, klabu kupitia Msola tutatoa tamko rasmi. . uongozi kwa pamoja tutafuatilia na taarifa rasmi kama klabu tutatoa baadaye ila wana Yanga wawe na amani kila kitu kinaenda sawa. . Yanga tuna utaratibu wetu wa kutoa taarifa na tutatolea ufafanuzi wa sintofahamu zote ikiwemo swala la wachezaji ambao sauti zao zimevuja. . swala la mikataba ni too personal hatutoweza kuweka wazi ila tuna wachezaji ambao wamemaliza mkataba na majadiliano yanaendelea kumjadili mchezaji mmoja mmoja ni kama kumpa kiki, hatuwezi kujadili mchezaji mmoja mmoja tutakuja na taarifa ya wachezaji wote. . ni kawaida wachezaji kuibua sintofahamu kipindi cha usajili ili kuongeza thamani yao sisi hatutishwi na hilo" David Luhago ( Katibu Mkuu - Yanga SC)


Sidhani toka Yanga izaliwe kama imewahi kuwa nankatibu poyoyo na asiye na uwezo hata Wa kueleza mambo kama huyu. Yaani anaongea utadhani anasutana na mtu au watu. Kwa kifupi anavyoongea anaudhi badala ya kushawishi
 
Wameanza kuondoka mmoja mmoja....
🚴🚴🚴🚴🚴

Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga SC Richard Shija amejiuzulu nafasi yake.

....
"Nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga.

Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea.

Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele"

*YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO*

*Shija Richard Shija*
 
GUMBO NAYE AJIUZULU YANGA :
Mimi Rodgers Gumbo leo Tarehe 27/03/2020 nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu nafasi zangu zote za uongozi ndani ya Yanga.

Yanga ni taasisi kubwa kuliko mimi Gumbo hivyo basi katika kuwajibika kwangu aidha niwe nimefanya au sikufanya kosa nimeamua kukaa pembeni ya Uongozi ili kuiacha Yanga ikiwa salama.

Sitazungumza chochote ila naamini ipo siku ukweli utajulikana.

Nitabaki kuwa Mwanachama mtiifu kwa Maslahi ya Yanga.
 
Nafikiri hofu imewatanda
Wameona hakuna aliyeko upande wao.

Walivyovihoji vinaeza kuwa na msingi ila muda waliowasilisha hivyo wanavyovihoji ndio umefanya waonekane ni watu wa ajabu sababu kwa sasa GSM ndio anayeplay part kubwa ndani ya Yanga. Na wao wapo tu.

Au kipo ambacho walikuwa wanafanya sie hatujui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…