"Kikubwa nnachoweza kusema nawaomba wana Yanga tuwe watulivu, klabu kupitia Msola tutatoa tamko rasmi. . uongozi kwa pamoja tutafuatilia na taarifa rasmi kama klabu tutatoa baadaye ila wana Yanga wawe na amani kila kitu kinaenda sawa. . Yanga tuna utaratibu wetu wa kutoa taarifa na tutatolea ufafanuzi wa sintofahamu zote ikiwemo swala la wachezaji ambao sauti zao zimevuja. . swala la mikataba ni too personal hatutoweza kuweka wazi ila tuna wachezaji ambao wamemaliza mkataba na majadiliano yanaendelea kumjadili mchezaji mmoja mmoja ni kama kumpa kiki, hatuwezi kujadili mchezaji mmoja mmoja tutakuja na taarifa ya wachezaji wote. . ni kawaida wachezaji kuibua sintofahamu kipindi cha usajili ili kuongeza thamani yao sisi hatutishwi na hilo" David Luhago ( Katibu Mkuu - Yanga SC)
Sidhani toka Yanga izaliwe kama imewahi kuwa nankatibu poyoyo na asiye na uwezo hata Wa kueleza mambo kama huyu. Yaani anaongea utadhani anasutana na mtu au watu. Kwa kifupi anavyoongea anaudhi badala ya kushawishi