Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Katika hali ya kusikitisha kama sio ujasiri klabu ya yanga imetangza rasmi kutoingiza timu uwanjan wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wa YANGA wakiwa na msemaji mkuu wa yanga l sendeu wamesema waliwapa taarifa toka jana TFF kwamba wamechoka na upuuzi wa kuibiwa hata wao wako kibiashara zaidi alisema sendu

Katika hali ya kusikitisha sendeu anasema hawa jamaa walitupa cheki mara mbili na zote zimebounce akuna hela

sasa unajiuliza hela zatu zimeenda wapi???na si hapo akasema walifwatilia fedha za mchezaji golikipa bora bwamdogo

yaw walipozitumia wakaanza kudai wanataka aje mwenyewe yaw amefika anazaidi ya miezi kadhaa na nikikwambia
amekwenda zaidi ya mara kumi pale TFF wanadanganya na huyu mhuni wao sijui boniface mi nasema leo lazima kieleweke
na wasifikirii YANGA ni wapuuzi wa ktumiwa kwenye biashara zao mwisho wa siku wanatuacha tunateseka

akisimulia kwa uchungu kiongozi mwingine amesema walishatabainisha TFF na kwa kuwa mpaka sasa awajatuletea hela zetu milion 15.5
na za yaw million 2.7 wakidai wamezila wanatafuta sasa sisi tunatangaza rasmi leo atacheza SIMBA VS TENGA/BONIFACE WAMBURA
Sisi lazima wajue hawa wachezaji wanafamilia zao na wanaishi kutokana na mpira tunapowaambia kila siku atujapewa hela zetu wanatuona wahuni na kwakuwa wao ndio wanacheza wameamua sasa waangalie hizo hela watapataje kwanza alisema sendeu
 
Kama mchezo huu una mgao kwa klabu ni bora kucheza waingize mapato hata kama hayatalipwa leo lakini bado watakuwa wanadai hata wakienda benki kukopa deni toka TFF ni mojawapo ya dhamana yao kukubaliwa kukopeshwa.

Wakigomea mchezo watabaki wanadai hizi TShs. 15.5 lakini wakicheza watakuwa wanadai zaidi ya TShs. 15.5; lakini kama hakuna mgawo bora wachezaji wakapumzika maana wakiumia na wakati TFF hawalipi madeni klabu itashindwa kuwahudumia kimatibabu.
 
Bora wanayanga msiingie uwanjani tu... Haiwezekani mpira ambao na ajira za vijana wetu uongozwe kwa ujanjaujanja!. Viva Young Africans Football Club....
 
kwa nini hawakuweka wazi muda mrefu kama hawataingiza timu kama hawajalipw pesa zao za awali ... maana hadi sasa watu watakuwa na ticket mkononi
 
Hivi hawa tielfuelfu peasa wanazopata wanafanyia nini.

Maana wanatangazaga mapato makubwa lakini madeni madogo madogo hawalipi hivi kweli mpira utaendelea?

Sasa nao yanga jana si waliweka mfukoni pesa ya BIG Bon wanataka kuingia nbayo mtini nini?
 
Timu zinaingia gharama kubwa sana katika maandlizi Kuzikutanisha yanga na Simba ni gharama kubwa. Tumu zinaingia gharama kwa maandalizi binafsi hata mechi zikiwa za kirafiki.

TFF naona sasa wamekuwa matapeli na walistahikh kabisa kuwafikisha mahakamani

T
 
tatizo TFF wanafanya mambo yao kwenye karpet hayako wazi .. maana kama kila kitu kikiwa wazi hakuna uhuni
 
Hao Yanga ni waoga tu hawana lolote! Kuna mwana-Yanga mmoja kanitonya kwamba baada ya kuumia Yaw Berko wana wasiwasi wa kupoteza mchezo.
 
Hivi hawa TFF wataendelea kuwafanya Yanga shamba la bibi mpaka lini? Tulidhani TFF kuongozwa na wataalam wa soka itakuwa yenye maana kuliko ya akina Michael Wambura, kumbe wote ni walewale tuu.

Inasikitisha sana na kwa nini siku zote iwe hela za Yanga tuu? Kukaa sana madarakani nadhani nalo ni tatizo, Tenga inabidi sasa ajivue gamba.
 
kwa taarifa yenu yanga wanataka kuvuruga ari na saikologia ya wachezaji wa simba,wataingiza timu dk za mwisho! Wanaendelea na maandalizi ya mwisho!

Simba wazuie wachezaji kufatilia ya yanga na tff ni mbinu tu!
 
simba wako vizuri mno ila tishio la yanga kujitoa litashusha morali plus yanga watataka bao la mapema kuwamaliza nguvu! Simba tukae chonjo,ezekiel upo?
 
sidhani kama ni busara, napita tu naelekea kuleee kwenye siasa, nikasimama kidogo hapa nipumzike maana michezo inaburudisha, kumbe nayo sasa imekua siasa tupu, kweheri ngoja nikacheki kwenye jukwaa la mahusiano labda siasa bado hazijafikishwa huko.
 
Warudishe mil 84 walizochukua alafu ndio wagome kuingiza timu uwanjani,mbona mnafanya kiini macho rudisheni pesa za watu ndio wagome, watacheza SIMBA NA TENGA, ANGETILE, MGONGOLWA, KAYUNI
 
Huu upuuzi kila siku tunausikia yani sijui tutaendelea lini..haingii akilini kabisa!! kwanini msiwalipe hizo pesa mnafanyia nini? halafu mnataka waingie tena uwanjani..huu si unyonyaji tena nje nje! acheni hizo bana
 
simba wako vizuri mno ila tishio la yanga kujitoa litashusha morali plus yanga watataka bao la mapema kuwamaliza nguvu! Simba tukae chonjo,ezekiel upo?
Yanga watapeleka timu amini usiamini hii ni janja ya nyani
 
Laikini hawa TFF nao, mbona wababaishaji hivi?
Ufisadi kila pahala.
 
madai ya yanga ni ya msingi sana,na wamewaumbua TFF,ila kama nilivyosema kupitia kuwatisha TFF wanataka kuwamaliza simba kisaikologia! Mtawaona uwanjani dk za mwisho kabisa! Mbinu za kizamani hizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…