Hongereni sna wana Yanga wezangu kwa ushindi huu wa leo......
Leo nilikwa uwanjani na nimeshuhudia timu yetu ikiibuka na ushindi licha ya Hamis Kiiza kukosa penati....
Pamoja na ushindi nina machache ya kuongea.....Kwa kweli timu yetu ni mbovu sana, mpira wetu ni mbovu sijapata kuona.....Wachezaji wetu wanacheza hovyo hovyo,hawana stamina,wanaanguka hovyo uwanjani....Hapa namkumbuka mtaalamu Sam Timbe...Huyu alikuwa akiwapa wachezaji mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kuwajenga kistamina kiasi cha kuchukwa na wachezaji,Timbe alikuwa mkali sana kwa wachezaji ukilinganisha na Kostadin Papic...Papic anapendwa na wachezaji kwa sababu tu anawalea na hawapi mazoezi ya nguvu, hili ni kosa kubwa sana.....
Kwa kiwango nilichokiona leo nachelea kusema kwamba Yanga hatujawiva kabisa kucheza na Zamalek,timu yetu haipo vizuri kimbinu,kistamina(kimwili) na kisaikolojia......Yanga hatuna washmbuliaji wazuri wa kumalizia,hawa Mwape na Asamoah ni magarasa,ni bure kabisa....Sijui ni kwa nini kocha anawaacha benchi Pius Kisambale,Shamte Ally na Jerry Tegete, hawa ni wazuri sana kuliko hata hao Mwape na Asamoah......Yanga bado tuna tatizo la beki wa kati wa kusaidiana na Nadir pamoja na beki wa kulia......Chuji bado mzito sana na nina wasiwasi sana katika mechi na Zamalek,anaweza kuwa uchochoro...Kwenye kiungo tupo vizuri hasa kwa Haruna Niyonzima,Juma Seif Kijiko na Nurudin Bakari(naomba apone haraka ili cheze mechi na Zmalek)......Hamis Kiiza ni mzuri sana ukilinganisha na Mwape na Asamoah.....Kwa magolikipa naona Kado karudi kwenye fomu yake maana leo kaokoa magoli matatu ya wazi kabisa.......
Tuombe Mungu Zamalek wasitufunge mengi hiyo jumamosi.......
Yanga: Daima mbele,Nyuma mwiko...