Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mkuu identity yetu ni wings zifanye kazi zaidi sasa hadi sasa wings zimeengeneza nafasi ngapi za wazi? Tuna winga wawili Wa nguvu Farid na Tuisila cha ajabu kila mechi ya ushindani mwalimu anampanga Fernandez winga ilihali hana nguvu,hana speed na hasaidii defense. Na hata kupitia hyo identity yetu bado huwa tunatengeneza nafasi vizuri tu toka kati sasa Leo kila kitu hakiwezekani na mwalimu kakaa na timu kwa mwezi mzima hakuna hata dalili ya mwangaza!?
 
Kama WACHEZAJI wazuri mbona kocha kafukuzwa?
 
Kama ni hivyo basi alipaswa awe ameshafika au tumeshatangaziwa atafika lini mana yeye maongezi yalishafanywa kitambo kabla ya kukwama dk za mwisho. Sasa cha ajabu wiki yote itaisha mwalimu hajafika
Uko sahihi, ngoja tuone mwisho wake mkuu
 
Sijui ila naweza sema hata wings hamtumii, nyinyi mnapiga mpira mbele mengine yatajulikana huko huko ,

Ukiondoa Ngassa aliekua kwenye ubora wake pamoja na Msuva, hamna winga mwingine ambae mnaweza jivunia kwamba mlikua nae

Wekeni kwanza misingi, la sivyo mtapotea sana, mfano saiv mmetimua kocha anapira bovu, sawa, ila mpira wenu mzuri ni upi?? swali gumu, atakuja kocha mwingine, unampa task gani? yakakwe binafsi au ataikuta Clubun??

Wakati kishingo anakuja alianza leta ujinga tukamwambia mpira wetu uko hv, faster tu kaisimamisha timu na matokeo anapata mazuri tu, sasa nyinyi mtamwambia mpira wenu ni upi? au aige kama upande ule?

hakuna shortcut, jipeni muda undeni kikosi
 
Ila siku akifungwa na Yanga ndipo utaelewa!
 
Ila siku akifungwa na Yanga ndipo utaelewa!
Kosa jingine kwa mindset za washabiki wa soka wa Simba na Yanga. Ubora wa timu zetu tunazipima kwa kushinda au kushindwa kwenye mechi za Kariakoo derby!!!! Yaani hapo ndio mpira wetu unapoanzia na unapoishia🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…