Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ukumbuke tu kuwa hiyo michezo yako mitatu ni dhidi ya Namungo, Azam na Dodoma jiji ambao tayari Yanga wameshamalizana nao raundi ya kwanza.
Na ukumbuke tuu ivyo viporo vimefutwa Simba itaendelea na ratiba nyingine za mechi izo za viporo tutakua hatua ya makundi
 
Hivi kwa nini michezaji yenu (Kaseke) hamuifundishi iwe professional. Mchezaji anaamini kuwa hapati goli kwa sababu ya kulogwa. Poor utopolo.
 
Leo nimeshangaa sana Kaseke na mwenzake kwenda goli la mpinzani kuanza kutikisa nyavu kama wanatafuta kitu hivi kwa chini,baadaye wakaenda hadi kwenye taulo la golikipa na kulikung'uta!Nilipigwa na butwaa kuona hivyo!Wakati huo Matokeo yakiwa Prison 1-0 Yanga na Yanga walikuwa wakishambulia sana!

Hii tabia si nzuri hasa kwa timu inayoshiriki ligi kuu na Club kubwa kama Yanga!Mnatia aibu kwakweli na hii sio mara ya kwanza ninyi kufanya hivyo!

Prison mnalingana nguvu maana kwenye mechi ya kwanza mlitoka sare tena kwenu!Sasa mnachoshangaa ni nini wao kuongoza kwa goli moja na ninyi mkiwa mnakosakosa?

Aibu kwenye michezo,mechi zinaonekana mpaka nje ya nchi halafu mnafanya ujinga!Shwain kabisa!



Siku nyingine mkagoma kuingilia lango la kuingia uwanjani,ninyi watu gani?Mbona mnaupa sana promo ushirikina?



Nawatakia kheri ya mwaka mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…