Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Je Yanga walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Kisheria walikuwa sawa na walikuwa na haki ya kusimamia msimamo wao. Kumbuka walijiandaa kwa muda wa awali.

Je Simba walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Walichofanya ni kutii agizo la TFF ambao ni wasimamizi wa ligi.

Je TFF walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa NDIYO. Walipokea maagizo kutoka Wizara inayosimamia michezo. Kumbuka Serikali yoyote ipo kwa ajili ya usalama na maslahi ya raia wake.

Kama wote walikuwa sahihi, Je nani abebe lawama?? Je ni Wizara?? Hapana! Ninaamini maamuzi yalifikiwa kwasababu ya maslahi ya raia, ni mapema sana kulaumu bila kujua sababu.

Je busara ilipaswa kutumika? NDIYO. Lakini swali lingine litakuja, Je wahusika walihusishwa katika maamuzi yaliyofanyika kabla ya kutaka watumie busara??

Simba na Yanga ambao ni wahusika wakuu hapa, walisikilizwa maoni yao kabla muda haujasogezwa mbele?? Kama hawakuhusishwa katika kufanya maamuzi, basi busara haikutumika. Kivipi utake busara kutoka kwao kama wewe hukutumia busara??

Maswali yote haya ni magumu, yanayohitaji majibu magumu ambayo kwasasa hayataleta suluhu. Swali moja la msingi lililobaki sasa ni,

Nini kifanyike??

Mechi imeshaota mbwawa, aibu imeshatokea, hasara kubwa imeshapatikana, limebaki suala moja la msingi, NINI KIFANYIKE??

Mechi itarudiwa?? Kama itarudiwa kwa gharama za nani?? Hasara iliyopatikana nani anaifidia?? Vipi kuhusu mashabiki??

Tafaruku yote hii inajibiwa kwa swali moja la msingi, NINI KIFANYIKE??
 
Hoja mfu za Haji Manara, kama kawaida yake anatanguliza Usimba mbele katika kutaka kuonesha kuwa wanastahili pongezi. Swali ni kwamba walikubali maelekezo ya TFF kwa kanuni zipi za mpira?. Pili atuambie wao kama Simba walishirikishwa kwenye uamuzi wa kupeleka mda wa mchezo mbele? Kama walishirikishwa, je waliwaona wawakirishi wa Yanga katika kikao hicho? Kama wawakirishi wa timu zote walikuwepo, je ni yapi walikubaliana?
Anaposema mchezo wa Yanga na Azam, Yanga na Biashara ulisogezwa mvele kwa kuzingatia matakwa ya kanuni. Mchezo wa Yanga na Azam ulisogezwa mbele masaa arobaini na nne kabla ya mchezo. Pia Yanga na Biashara ulisogezwa mbele masaa ishirini na nne kabla ya mchezo na hivyo ndio kanuni zinataka.
Kusogeza mcheza wa Yanga wakati, Yanga wakiwa katika maandalizi ya mwisho ya kuja uwanjani ni kutaka kuwahujumu Yanga.
Kwa andiko hili lake, anatupa sisi wapenzi wa mpira kuwa kuna kitu Simba ilikuwa inakijua na ndio maana hawakufika uwanjani kwa mda pangwa. Labda Simba kwa pamoja na TFF walipanga kwa pamoja kuihujumu Yanga
 
Habari za chini chini zinasema alihusishwa Injinia
Akaridhia lakini ishu ilipofika kwa msola akagoma nae akataka pia kumuonyesha Injinia kwamba yeye pia ni mwenyekiti
Kwa upande mwingine Vita ya Jana pia imehusisha
VIONGOZI VS GSM
 
YANGA NDIO WAMEIBUKA WABABE KWENYE SAKATA LA DABY YA KARIAKOO, WAMEZIVUA NGUO NA KUZIACHA UCHI SERIKALI, TFF NA BODI YA LIGI.

Bila kujali sababu ambazo hazijawekwa wazi za kusogeza mechi kwa saa mbili kutoka kwa serikali. Ila kwa hili Yanga wameibuka wababe na kudhihirisha wazi hakuna wa kuwazuia wakiamua lao.

Tff ni kama waliamua kunawa mikono na kuiachia serikali itoe majibu kwa lilitokea. Wanaposema ni maagizo ya Serikali maana yake wao waliamua hawataki kuchafuka na kuonyesha busara na kutiii mamlaka.

Simba pamoja na kuonekana ni waoga ila kimsingi nao walichokifanya ni utiii na busara kuheshimu mamlaka.

Yanga wao waliamua kutunishiana misuli, jeuri na kuonyesha ubabe kwa kisingizio cha kusimama kwenye kanuni, sheria na taratibu. Tujiulie walichokuwa wanakipigania Yanga ni kuheshimu kanuni pekee au kuna kitu kingine zaidi nyuma ya pazia? Yanga siku za karibu kuna mechi zao zilibadilishwa muda wa kuanza na hatukuona wakipinga na kusema kanuni ziheshimiwe. Kwa nini kanuni hii wanataka iheshimiwe kwa mechi moja tu? Au hii kanuni imetungwa Jana au juzi? Hapa ndipo tunapopata shaka kuna kitu zaidi ya kutaka kanuni iheshimiwe nyuma ya pazia.

Ni Wazi Yanga wametuonyesha na kutufundisha unaweza kuzichezea mamlaka upendavyo na mwisho ukaibuka mshindi. Yanga imesimamia kanuni ila kwa kuheshimu huko kanuni imezivua nguo na kuziacha uchi kwa aibu ya karne Serikali, Tff na Bodi ya ligi. Yanga wametufundisha hata ukiwa mdogo unaweza kumvimbia mkubwa na kumfedhehesha na kumtia aibu ilimradi uibuke mshindi na mbabe.
Kusogezwa mbele saa mbili kwa mechi ndio sababu ya sakata lote hili? Mimi siamini. Iwapo mashabiki tuliokuwepo uwanjani tena wengine tangu saa saba mchana tulivumilia na kukubali japo shingo upande kuvumilia huo muda na kusubiri mechi kwa Yanga ilishindikana nini?
Kimsingi Yanga ndio waliotuibia viingilio vyetu kwa kutaka waonekane Wababe mbele ya Serikali, Tff na Bodi ya ligi. Imani bado Yanga wangeamua kutumia hekima, busara na utiifu bado tusingefika kote huku.
YANGA NDIO WALIOIBUKA WABABE, KUONYESHA JEURI KWA YAO KWA MAMLAKA ZOTE ZA JUU YAKO KATIKA SAKATA ZIMA.
( Jicho la tatu la Mgalilaya).

Nimeona sehemu
 
The law should be respected by everyone. YANGA proved that no one's above the law. Even the Government TFF, board of trustees are obliged to adhere the laws.
 
Najua hiki ndo kimebakia Mtani kutuombea njaa.

Niseme tu ni mechi ngumu ila namini tutapata matokeo.
Kwa sasa Simba haina haja ya kuiombea Yanga njaa, maana tayari gap la point 4 na mechi 2 mkononi ni njaa tosha. Yanga ndio inatakiwa kuiombea Simba njaa. Kama kuna mwana Yanga ambaye bado anafikiria ubingwa, basi ana roho ngumu sana
 
Hivi kocha haoni hilo zigo Sarpong uwanjani? Aiseee kuna wachezaji wanakula hela bure tu Yanga,sioni sababu ya kuwa na mapro
 
Kweli Yanga ndiyo tumefika hapa kishangilia mbwembwe za Feisal badala ya magoli? Daaah aiseee
 
Dk ya 60,sioni tunaweza pata goli kupitia wapi, labda la bahati nasibu tu🙉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…