CARDLESS
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 7,840
- 15,918
Game za YANGA vs AZAM na YANGA vs BIASHARA ratiba zake zilitoka siku 3 kabla ya mechi husika na ni kama zinavyoonekana hapa chin..View attachment 1778065
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hoja mfu za Haji Manara, kama kawaida yake anatanguliza Usimba mbele katika kutaka kuonesha kuwa wanastahili pongezi. Swali ni kwamba walikubali maelekezo ya TFF kwa kanuni zipi za mpira?. Pili atuambie wao kama Simba walishirikishwa kwenye uamuzi wa kupeleka mda wa mchezo mbele? Kama walishirikishwa, je waliwaona wawakirishi wa Yanga katika kikao hicho? Kama wawakirishi wa timu zote walikuwepo, je ni yapi walikubaliana?Je Yanga walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Kisheria walikuwa sawa na walikuwa na haki ya kusimamia msimamo wao. Kumbuka walijiandaa kwa muda wa awali.
Je Simba walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa, NDIYO. Walichofanya ni kutii agizo la TFF ambao ni wasimamizi wa ligi.
Je TFF walikuwa sahihi?? Jibu langu litakuwa NDIYO. Walipokea maagizo kutoka Wizara inayosimamia michezo. Kumbuka Serikali yoyote ipo kwa ajili ya usalama na maslahi ya raia wake.
Kama wote walikuwa sahihi, Je nani abebe lawama?? Je ni Wizara?? Hapana! Ninaamini maamuzi yalifikiwa kwasababu ya maslahi ya raia, ni mapema sana kulaumu bila kujua sababu.
Je busara ilipaswa kutumika? NDIYO. Lakini swali lingine litakuja, Je wahusika walihusishwa katika maamuzi yaliyofanyika kabla ya kutaka watumie busara??
Simba na Yanga ambao ni wahusika wakuu hapa, walisikilizwa maoni yao kabla muda haujasogezwa mbele?? Kama hawakuhusishwa katika kufanya maamuzi, basi busara haikutumika. Kivipi utake busara kutoka kwao kama wewe hukutumia busara??
Maswali yote haya ni magumu, yanayohitaji majibu magumu ambayo kwasasa hayataleta suluhu. Swali moja la msingi lililobaki sasa ni,
Nini kifanyike??
Mechi imeshaota mbwawa, aibu imeshatokea, hasara kubwa imeshapatikana, limebaki suala moja la msingi, NINI KIFANYIKE??
Mechi itarudiwa?? Kama itarudiwa kwa gharama za nani?? Hasara iliyopatikana nani anaifidia?? Vipi kuhusu mashabiki??
Tafaruku yote hii inajibiwa kwa swali moja la msingi, NINI KIFANYIKE??
Habari za chini chini zinasema alihusishwa InjiniaHoja mfu za Haji Manara, kama kawaida yake anatanguliza Usimba mbele katika kutaka kuonesha kuwa wanastahili pongezi. Swali ni kwamba walikubali maelekezo ya TFF kwa kanuni zipi za mpira?. Pili atuambie wao kama Simba walishirikishwa kwenye uamuzi wa kupeleka mda wa mchezo mbele? Kama walishirikishwa, je waliwaona wawakirishi wa Yanga katika kikao hicho? Kama wawakirishi wa timu zote walikuwepo, je ni yapi walikubaliana?
Anaposema mchezo wa Yanga na Azam, Yanga na Biashara ulisogezwa mvele kwa kuzingatia matakwa ya kanuni. Mchezo wa Yanga na Azam ulisogezwa mbele masaa arobaini na nne kabla ya mchezo. Pia Yanga na Biashara ulisogezwa mbele masaa ishirini na nne kabla ya mchezo na hivyo ndio kanuni zinataka.
Kusogeza mcheza wa Yanga wakati, Yanga wakiwa katika maandalizi ya mwisho ya kuja uwanjani ni kutaka kuwahujumu Yanga.
Kwa andiko hili lake, anatupa sisi wapenzi wa mpira kuwa kuna kitu Simba ilikuwa inakijua na ndio maana hawakufika uwanjani kwa mda pangwa. Labda Simba kwa pamoja na TFF walipanga kwa pamoja kuihujumu Yanga
Najua hiki ndo kimebakia Mtani kutuombea njaa.Zinadodoka nyingine
Kwa sasa Simba haina haja ya kuiombea Yanga njaa, maana tayari gap la point 4 na mechi 2 mkononi ni njaa tosha. Yanga ndio inatakiwa kuiombea Simba njaa. Kama kuna mwana Yanga ambaye bado anafikiria ubingwa, basi ana roho ngumu sanaNajua hiki ndo kimebakia Mtani kutuombea njaa.
Niseme tu ni mechi ngumu ila namini tutapata matokeo.
0-0 dk 63Ngp hapo