Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Aione kwenye file Shadeeya
 
Hakika usemalo Mkuu.

Lakini hivi vilabu yetu bana usije kuta kikosi anapangiwa na watu yaani kwamba kuna watu fulani ni lazima wacheze iwe isiwe.

Halafu hivi yule Moloko ulimwelewa? [emoji853]
Hamna la maana alichokuwa anafanya, kashindwa kuvaa viatu vya Kisinda. Kisinda angekuwepo, mabeki wa Rivers wasingepanda mbele kutengeneza mashumbulizi lakin yeye anaanguka anguka tu na kupenda kukaa na mpira halafu wapinzani wana iwin Mechi ya marudiano kocha afanye mabadiliko. Makambo na Yusuph Athuman wapewe nafasi. Makambo ana kitu na huyu dogo pamoja na dakika chache alizocheza kaonesha ni mchezaji anaweza kuisadia Yanga mbele tofauti na yacouba. Naomba Aucho na Djuma shabani ITC zao ziwe fresh ili mechi ya marudiano wawepo. Zawadi mauya akae nje kwanza shuguli za kimataifa aiwezi. Bangala pia naomba awepo maana kwenye wiki ya wananchi kacheza dakika chache lakini nimemuona ni bonge la mchezaji hakuna mcheza wa kibongo anayeweza kumweka benchi. Moloko awekwe benchi kwanza nafasi yake iangaliwe mwingine wa kucheza hata Dickson Ambundo au Kaseke. Mechi bado hii endapo kocha ataweza kupiga hesabu vizuri Yanga inauwezo wa kupindua meza kwasababu Yanga inayo wachezaji wazuri japo bado timu haijawa nzuri. Mechi ya marudiano inabidi tuwe vizuri kwenye ukuta, viungo wawe wazuri, kocha afanye uchaguzi mzuri wa playmaker na mwisho kabisa washambuliaji watumie nafasi chache zitakazopatikana. Nimeshangaa jana timu hata kufanya pressing hamna, kufanya marking hamna, wanawasindikiza tu wachezaji huku wanageuzwa geuzwa kama chapati.

Nafasi bado ipo endapo kocha atafanya selection nzuri ya wachezaji, mbinu iliyokuwa sahihi na pia kama Djuma na Aucho watakuwepo.
 
Kwa Nigeria sidhani aisee.

Hivi bro ikawaje yule Moloko kocha akamwacha kucheza 90mins au mie ndo sikumwelewa mana saa ingine anachokifanya alikuwa anakijua mwenyewe?
Kuweni wapole tu tengenezen timu na iheshimuni Simba sc
 
Kocha Nabi anazingua, Mi napendekeza team apewe Charles Boniface Mkwasa msaidizi awe Nsajigwa, Wanaijeria hawachomoki hapo.
 
Yaani kuna vitu vingi kiasi kwamba ukianza kulaumu utalaumu uongozi,benchi la ufundi na wachezaji pia Mana wote wana makosa japo Mimi lawama kuu napeleka kwa uongozi kisha benchi la ufundi hususana Mwalimu na kisha wachezaji!

UONGOZI
-ITC za wachezaji watatu zimeleta shida sana. Kwanza niliamini lengo la usajili Wa wale wachezaji ni kuongeza ukubwa Wa kikosi chetu na pia kuongeza weledi Wa timu yetu ktk michuano ya kimataifa mana wale wachezaji wote wana uzoefu mkubwa. Kitendo cha kukosekana kwa wale wachezaji watatu kulifanya kikosi chetu kisiwe na tofauti kubwa na kile cha msimu ulopita. Mimi niliamini hawa wachezaji wamessjiliwa hasa kwa ajili ya mashindano makubwa hasa kama haya ya CCL mwisho Wa siku viongozi wanatuambia tusiwe na wasiwasi hata kama hawatacheza CCL kwenye ligi watacheza[emoji16]

-Kambi ya Morocco ilikuwa na tija gani? Nani aliyeratibu ile kambi bila kujua ratiba za klabu? Au kulikuwa na masilahi ya watu binafsi?

-Kuhusu kukosekana kwa hizo ITC kwa wakati kuna mambo mengi ya kujiuliza kiasi kwamba kiujumla naweza hitimisha kwamba tuna viongozi wababaishaji sana n.k

KOCHA
Timu bado inacheza vibaya wakati keshakaa na timu kwa muda Wa miezi 4 hadi sasa. Upangaji Wa kikosi cha kwanza ni Wa mashaka,ufanyaji Wa mabadiliko ni Wa mashaka. Hapa Nina mashaka na uwezo Wa kocha(Hata alivyoletwa siku ya kwanza nilihoji vigezo gani vilitumika kumleta wakati profile zake za huko alikotoka zinaonyesha ni mbovu?). Hawezi jitetea kwamba timu ilicheza bila uelewano sababu wachezaji hawajakaa pamoja muda Wa kutosha wakati ktk kikosi alichokitumia wachezaji wageni walikuwa wawili tu n.k

WACHEZAJI
-kutotumia nafasi wanazozipata(mf. Yacouba 3, Feisal 1, Makambo 1 na Yusuf 1)
- Kutojitoa sana japo siyo wote mana wapo walionyesha kupigana sana na wengine kuchukulia poa tu n.k

MWISHO
Kule Nigeria tunapaswa kwenda mapema ili tukakabiliane na hujuma zao na tuzishinde au tuendane nazo. Baada ya hapo siku ya mchezo timu yetu ikajitume sana kuanzia mwanzo hadi mwisho,tukaanze na kuwashambulia kama hatuna cha kupoteza Mana tushapoteza ili tuwachanganye na Mungu akijaalia tupate goli la kuturudisha mchezoni. Wachezaji wasipaniki ili kutoka mchezoni na kuepuka kadi

Kikosi changu(kwa options zilizopo)
Diarra
Kibwana
Bryson kama hayupo basi huyo huyo Adeyum
Job
Bakari
Bangala
Mukoko
Moloko
Feisal
Makambo
Kaseke

Lolote laweza tokea japo wao kwa kiasi kibubwa sana wana nafasi nzuri kuliko sisi!
 
Djuma, Aucho na Mayele hawatocheza labda ikitokea tukavuka hizi raundi na kuingia makundi ndipo tunaweza tumia zile nafasi ambazo CAF hutoa kwa timu kuongeza wachezji
 
Vema ndugu!
 
Kwa Nigeria sidhani aisee.

Hivi bro ikawaje yule Moloko kocha akamwacha kucheza 90mins au mie ndo sikumwelewa mana saa ingine anachokifanya alikuwa anakijua mwenyewe?
[emoji23][emoji23][emoji23] acha nipite kimya kimya tu bado tunaomboleza msiba wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…